Dora amkubali kinoma noma Tambwe

Muktasari:

  • Msanii wa filamu nchini ameweka wazi namna anavyokubali uwezo wa Amissi Tambwe kwamba ni mchezaji ambaye ameliheshimu soka na lenyewe limemheshimu.

Dar es Salaam.Mcheza filamu Wansukula Zakaria ‘Dora’ humwambii kitu kuhusiana na mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe anamkubali kinoma noma.

Dora hajaficha yeye ni Yanga lialia na shabiki Tambwe anayempenda kutokana na juhudi yake uwanjani, inayomtofautisha na wengine.

"Tambwe ni mchezaji anayejituma kwa bidii uwanjani, alianza kuonyesha tangu akiwa Simba na amelithibitisha hilo na Yanga, napenda jinsi ambavyo anaonyesha uwezo wake.

"Soka linamheshimu kwa sababu ameliheshimu ndio maana akipata nafasi ya kucheza anaonyesha uwezo wa hali ya juu na msimu huu kwa sababu ya majeruhi ndio maana hajacheza.

"Naamini msimu huu angekuwa vizuri basi angekuwa katika kinyang'anyiro cha ufungaji bora kama ilivyo kwa Meddie Kagere, amemaliza na mabao 23," alisema Dora.