Dismas Ten awapiga kijembe Simba kimtindo

Tuesday June 11 2019

 

By Thomas Ng'itu

Dar es Salaam. Afisa Habari wa Yanga, Disma Ten amewapiga vijembe watani wao wa jadi (Simba) kwa kuachia picha za usajili wa wachezaji wao wa zamani huku wao wakiwa wanaachia wapya.

Simba imesambaza picha za wachezaji wao John Bocco (jana) na Aish Manula (leo) wakiwa wanasaini mikataba mipya ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili.

Ten aliyasema hayo wakati akielezea kuhusu tukio la klabu yao kubwa kuliko ndio alisema hivi sasa siyo muda wa picha za zamani zaidi ya tukio lao ndio lizungumziwe.

"Tunataka tutikise nchi kwa sababu Yanga ni timu kubwa nchini kwa hiyo tunaamini kabisa tukio letu ni kubwa kama ambavyo jina lenyewe lilivyo," alisema Ten.

Tukio hilo la kubwa kuklko linafanyika Juni 15 kwa lengo la kuchangisha pesa za kuanyia usajili wa wachezaji watakaoukuwa katika kikosi hiko msimu ujao.

Advertisement