Dele Alli ashusha presha kuhusu kocha Pochettino

Muktasari:

Presha ilishuka kidogo baada ya Jumanne iliyopita kushinda 5-0 dhidi ya Red Star Belgrade kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni ushindi wao wa kwanza kwenye michuano hiyo kwa msimu huu, lakini ni wa nne katika mechi 13 zilizopita.

LONDON ,ENGLAND . DELE Alli amsema mastaa wa Tottenham Hotspur wote kwa asilimia 1,000 wanamuunga mkono kwa kila kitu kocha wao, Mauricio Pochettino ambaye kwa sasa anadaiwa kukalia kuti kavu huko London.

Kocha huyo Muargentina amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na Spurs kupata matokeo ya hovyo uwanjani.

Presha ilishuka kidogo baada ya Jumanne iliyopita kushinda 5-0 dhidi ya Red Star Belgrade kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa ni ushindi wao wa kwanza kwenye michuano hiyo kwa msimu huu, lakini ni wa nne katika mechi 13 zilizopita.

Alipoulizwa kama wachezaji wanamsapoti kocha wao, Dele alisema: “Ndio, asilimia 1,000.

“Wengi wetu tusingekuwa hapa tulipofika kwa sasa kama isingekuwa yeye. Sote kitu ambacho tunapaswa kufanya ni kumshukuru tu.

“Siku zote tumekuwa tukimwaamini kwa asilimia 100 na tunaendelea kufanya hivyo.”