Chelsea yachomoa, Mourinho arusha ngumi

Muktasari:

Manchester United wameshindwa kupata ushindi wowote Stamford Bridge tangu Sir, Alex Ferguson alipostaafu soka mwishoni mwa msimu wa 2012-13. Wametoka sare mbili na kupoteza mechi tano.

London, England. Ross Barkley amefunga bao la kusawazisha katika dakika sita za nyongeza na kuisaidia Chelsea kulazimisha sare 2-2 na Manchester United, huku Jose Mourinho akitaka kurusha ngumi.

Kuingia kwa bao la kusawazisha la Chelsea kulisababisha kocha Marco Ianni kushangilia kwa nguvu mbele ya benchi la Manchester United, jambo ambalo iliyomkera Mreno huyo na kuanza kumkimbiza.

Vurugu hizo zilidumu kwa dakika mbili kabla ya mchezo huo kuendelea na mwamuzi kumaliza pambano matokeo yakiwa 2-2.

Beki Mjerumani Antonio Rudiger alifunga bao la kwanza kwa kichwa akimalizia mpira wa kona na kumkuta mfungaji akiwa peke yake na kumalizia mpira wavuni.

Manchester United ilikwenda katika mchezo huo wa leo Jumamosi ikiwa na rekodi ya kushinda mechi moja kati ya 16 ilizocheza Stamford Bridge ilibadilika kipindi cha pili.

Mshambuliaji Anthony Martial alifunga bao la kusawazisha akiunganisha krosi ya Ashley Young kabla ya kupiga shuti kali akiwa umbali wa mita 15, lililompita kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga na kuifanya Man United kuongoza kwa mabao 2-1.

Hata hivyo, Barkley alinusuru Chelsea kwa kipigo baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya David Luiz na kuwasawazishia wenyeji.