Chapa Dimba yamleta Luis Garcia Kenya

Thursday June 13 2019

 

By Fadhili Athumani

Nairobi. Winga wa zamani wa Liverpool na Barcelona, Luis Javier Garcia atahudhuria fainali ya makala ya pili ya mashindano ya kuvumbua vipaji ya Chapa Dimba na Safaricom, yanayotarajiwa kufanyika ugani Kinoru, katika kaunti ya Meru, kuanzia Juni 20 hadi Juni 23.

Gwiji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania, ambaye ni Balozi wa LaLiga, ambao ni washirika wa mdhamini mkuu wa mashindano hayo, kampuni ya simu ya Safaricom, ataendesha kliniki ya michezo nchini, kisha atahudhuria mechi za nusu fainali na fainali.

Kwa mujibu wa utaribu wa mashindano hayo, yameingia mwaka wake wa pili, timu nane za wanaume na nane za wanawake, kutoka mikoa nane zitachuana kuwania ubingwa wa taifa, zawadi ya pesa taslimu shilingi milioni moja, simu na muda wa maongezi.

Garcia, alichezea klabu kubwa za Ulaya ikiwemo Barcelona na Atletico Madrid. Alicheza mechi 150 za LaLiga na kufunga mabao 22. Aliwakilisha timu ya taifa ya Hispania mara 20, ikiwemo fainali ya Kombe la Dunia ya mwaka 2006, mwaka mmoja baada ya kutwaa taji la ligi ya mabingwa Ulaya na klabu ya Liverpool.

“Tunapenda kuchukua fura hii, kuwashukuru sana wenzetu LaLiga kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakitupatia. Ujio wa Luis Garcia utasaidia kuongeza hamasa kea vijana wetu na soka la Kenya. Tunapenda kuwaomba vijana wote watakaokua Meru, kuhudhuria kliniki atakayoiendesha Garcia na kujifunza zaidi,” alisema Mkuu wa Huduma kwa wateja wa Safaricomn, Sylvia Mulinge.

Fainali za kitaifa zitafanyika baada ya kukamilika kwa fainali za mikoa, zilizoendeshwa katika mikoa nane, na kuhusisha timu zipatazo 1,600. Makala haya ya pili, yalianza Oktoba mwaka jana, mechs zote zikiendeshwa kwa njia ya makundi. Lengo kuu la Chapa Dimba ni kukuza na kulea vipaji vya soka nchini.

Advertisement

 Ratiba ya Mechi za Chapa Dimba:

WASICHANA

Robo fainali ya kwanza: Acakoro Ladies (Nairobi) vs. NCOED (Nyanza)

Robo fainali ya pili: Changamwe Ladies (Coast) wamefuzu nusu fainali (hakuna mpinzani) 

Robo fainali ya tatu: St. Mary’s.Ndovea (Eastern) vs. Barcelona Ladies (Central)

Robo fainali ya nne: Archbishop Njenga (Western) vs. Kitale Queens (Rift)

 Nusu fainali ya kwanza: Mshindi robo fainali ya kwanza Vs Changamwe Ladies

Nusu fainali ya pili: Mshindi robo fainali ya tatu Vs Mshindi robo fainali ya nne

Fainali: Mshindi nusu fainali ya kwanza Vs Mshindi nusu fainali ya pili 

 WAVULANA

Robo fainali ya kwanza: Lugari Blue Saints (Western) vs. Super Solico (Eastern)

Robo fainali ya pili:  Euronuts (Central) vs. Manyatta United (Nyanza)

Robo fainali ya tatu:  Berlin FC (North Eastern) vs. Al Ahly (Rift)

Robo fainali ya nne: Shimanzi Youth (Coast) vs. South B United (Nairobi)

 Nusu fainali ya kwanza: Mshindi robo fainali ya kwanza Vs Mshindi robo fainali ya pili

Nusu fainali ya pili: Mshindi robo fainali ya tatu Vs Mshindi robo fainali ya nne

Fainali: Mshindi nusu fainali ya kwanza Vs Mshindi nusu fainali ya pili

Advertisement