Bocco, Kagere, Okwi waanzishwa pamoja

Muktasari:

Washambuliaji hao kwa pamoja wamefunga jumla ya mabao 10 kati ya 16 ambayo Simba imefunga katika mechi tisa ilizocheza ambapo Kagere na Okwi kila mmoja amefumania nyavu mara nne huku Bocco akifunga moja.

Washambuliaji Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco leo wameanza pamoja katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Simba ikiwa ni baada ya mechi tano kupita tangu walipoanzishwa hivyo.
Watatu mara ya mwisho walianzishwa kwenye kikosi cha kwanza Septemba 15 kwenye mchezo wa ugenini dhidi ya Ndanda ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Tangu hapo Simba ilicheza dhidi ya Mbao FC, Mwadui FC, Yanga, African Lyon, Stand United na Alliance FC bila watatu hao kuanza pamoja.
Katika kikosi cha kwanza kilichoanza leo dhidi ya Ruvu Shooting, Simba imefanya mabadiliko kadhaa kutoka kwenye kikosi chake kilichoanza ambacho kiliibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Alliance kwa kuwaweka benchi Said Ndemla, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Mohammed Ibrahim na Adam Salamba huku ambao nafasi zao zimechukuliwa na Bocco, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein, Shiza Kichuya, Kagere na Jonas Mkude.


Kikosi kilichoanza cha Simba ni Aishi Manula, Kapombe, Mohammed Hussein, Paschal Wawa, Juuko Murshid, Mkude, Okwi, Cletus Chama, Shiza Kichuya, Bocco, Kagere.


Kikosi cha Ruvu Shooting kinaundwa na wachezaji Abdallah Rashid, Abdul Mpambika, Mau Bofu, Renatus Ambrose,Tumba Swedi, Zuberi Dabi, Shaban Usala, Baraka Mtuwi, Said Dilunga, Fully Maganga, William Patrick