Bizimungu amjaza mbinu Aiyee

Muktasari:

  • Kuhusu ishu ya mchezaji wake kutoitwa kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Uganda, alisema hilo ameliweka sawa na mchezaji wake na kinachotakiwa ni kuongeza juhudi na kufunga tu.

KASI ya ufungaji ya mshambuliaji Salim Aiyee wa Mwadui, imekuwa kubwa kiasi cha kuwazidi washambuliaji wa kigeni Meddie Kagere (Simba) na Herieter Makambo (Yanga).

Aiyee mpaka sasa ndiye kinara akiwa amefunga mabao 15, huku Makambo na Kagere wakifuatia na mabao yao 12 kila mmoja.

Kocha mkuu wa Mwadui, Ally Bizimungu aliliambia Mwanaspoti anataka kuona straika huyo kuwa miongoni mwa mastraika bora nchini huku akimzidishia mbinu za kiufundi ili aweze kutikisa nyavu zaidi.

“Huwa ninamwambia Aiyee anapokuwa uwanjani akae eneo lake maalumu kwa sababu hata tukiwa mazoezini anafunga, mazoezi ndio hutoa twaswira ya kwenda kufanya vizuri kwenye mechi, hivyo tunachokitengeneza mazoezini ndichoo kinachoenda kufanywa wakati wa mechi,” alisema.

Kuhusu ishu ya mchezaji wake kutoitwa kikosi cha timu ya Taifa kinachojiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Uganda, alisema hilo ameliweka sawa na mchezaji wake na kinachotakiwa ni kuongeza juhudi na kufunga tu.

“Bado ana nafasi huko mbele ya kuitwa lakini nimemwambia na nitaendelea kumwambia afunge sana, halafu kuhusu kuitwa amwachie mwalimu kama ataona ana umuhimu basi atamwita,” alisema.