Birigimana anukia Alliance FC

Muktasari:

Baada ya kuona kwamba hajalipwa stahiki zake, mshambuliaji wa Stand UTD, Brigmana Blaise, ameamua kutimka klabuni hapo na kujiunga na kikosi cha Alliance.

Dar es Salaam. Mshambuliaji Birigimana Blaise wa Stand United anukia kujiunga na kikosi cha Alliance kinachonolewa na kocha Malale Hamsini.

Birigimana alikuwa akihusishwa kujiunga na Yanga, lakini Uongozi wa klabu hiyo ulimpotezea na sasa ameibukia katika kikosi cha Alliance.

Taarifa zilizopenyezewa Mwanaspoti ni kwamba mchezaji huyo ameshaanza kujifua na kikosi hicho mkoani Mwanza na amekipotezea kikosi chake cha Stand Utd kutokana na kushindwa kumlipa mishahara yake pamoja na pesa za usajili.

Pia, inatajwa kwamba mchezaji huyo amewasilisha malalamiko yake katika Shirikisho la soka nchini (TFF) ili usajili wake utakapofanyika kusiwe na pingamizi lolote.