Ben Pol hata muziki wa Injili yumo

Saturday September 8 2018

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Mwanamuziki bongo fleva, Ben Pol ameweka wazi kipaji chake hakina mipaka ndio maana amefanya kazi na wimbaji wa nyimbo za injili Paul Clement.

Msanii huyo alisema kazi yake ni kuimba na kuandika ujumbe ambao utakuwa na somo ndani yake kwa wanaousikiliza muziki wake.

"Kikubwa ni namna ya kupeleka ujumbe sehemu husika, mfano ninapoimba nyimbo za Bongo Fleva lazima niangalie wasikilizaji wa muziki wangu wanakuwa wanataka nini, lakini ninapokuwa na watu wa dini lazima ujumbe ubadilike.

"Tayari nina wimbo niliomwandikia Paul Clement unaitwa Amani na umepokewa vizuri na watu wake, hilo ndilo linanifanya kazi yangu isiwe na mipaka," alisema Ben pol.

Advertisement