Beki wa Chelsea, Zappacosta mbioni kujiunga Roma

Muktasari:

Zappacosta alijiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka minne akitokea Torino kwa paundi 23m mwaka 2017.

London, England. Beki wa Chelsea, David Zappacosta yupo mbioni kujiunga na AS Roma kwa mkopo.

Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Italia, alifika Roma siku ya Jumanne kukamilisha mpango huo.

Zappacosta alijiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka minne akitokea Torino kwa paundi 23m mwaka 2017.

Lakini amefanikiwa kucheza mechi 22, za Ligi Kuu, katika msimu wake wa kwanza alicheza mara nne tu mnamo 2018-19. Hakuonekana katika timu ya Chelsea msimu huu.

Beki wenzake David Luiz na Gary Cahill tayari wameondoka Stamford Bridge msimu huu.