Barcelona yamtuma Abidal kufuata Neymar PSG

Tuesday August 13 2019

 

Barcelona, Hispania.Mkurungezi wa ufundi wa Barcelona, Eric Abidal amesafiri kwenda Paris kwa ajili ya mazungumzo na PSG kuhusu Neymar baada ya mashabiki kumzoea huku Real Madrid wakijiweka mbali.

Abidal amekwenda Paris kwa lengo la kufanikisha suala la uhamisho wa nyota huyo kuugana tena na miamba hiyo ya Hispania.

Neymar amekaa kwa misimu minne Hispania akiwa na muunganiko mzuri na Lionel Messi na Luis Suarez akifanikiwa kutwaa mataji mawili ya La Liga pamoja taji la Ligi ya Mabingwa 2015.

Nyota huyo wa zamani wa Santos sasa yupo katika nafasi nzuri ya kuongeza idadi ya mabao kutoka 105 aliyofunga katika mechi 186 alizocheza Hispania.

Mashabiki wa PSG wameonyesha kuchoshwa na nyota huyo baada ya kubeba mabango yaliyoandikwa ondoka Neymar 'Neymar go away' wakati wa mchezo wao wa ufunguzi Ligue 1 walioshinda 3-0 dhidi ya Nimes.

Neymar aliondoka Barcelona kwenda PSG kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa pauni 198milioni mwaka 2017 kwa kipindi hicho amefanikiwa kucheza mechi 58 na kufunga mabao 51 kwa mabingwa hao wa Ligue 1.

Advertisement

Advertisement