Barcelona yaja na sizitaki mbichi hizi kwa Aubameyang

Wednesday March 25 2020

 

Madrid, Hispania. Barcelona imeweka pozi la kumsajili nahodha wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang katika usajili wa mwisho wa msimu huu.

Badala yake Barcelona inataka kujikita katika usajili wa nyota wa Inter Milan, Lautaro Martinez.

Wakati klabu hiyo ikimpa kisogo mshambuliaji huyo, Inter Milan inaweza kumpoteza Martinez.

Matumaini ya Aubameyang ambaye ni nahodha wa Gabon, kuongeza mkataba Arsenal hatua inayozipa nafasi klabu za Ulaya kumnyakua.

Barcelona inaonekana kuvutiwa na ubora wa Martinez kuliko Aubameyang ambaye amecheza kwa kiwango bora msimu huu akiwa Arsenal.

Mkataba wa mshambuliaji huyo unamalizika mwakani majira ya kiangazi na Manchester United inahusishwa na mpango wa kumsajili.

Advertisement

Licha ya Aubameyang mwenye miaka 30 kusisitiza ana furaha, lakini klabu yake hadi sasa haijafanya mazungumzo naye ya kuongeza mkataba.

Arsenal ilitoa kwa Borussia Dortmund Pauni 56 milioni kupata saini ya nyota huyo wa Gabon Januari, 2018.

Aubameyang amefunga mabao 20 katika mashindano yote msimu for 2019-2020. Mesut Ozil, Bukayo Saka, Shkodran Mustafi na Reiss Nelson mikataba yao inamalizika mwakani.

Advertisement