Balinya, Kipkirui waachiwa msala

Thursday March 05 2020
pic balinya

WAKATI Gor Mahia ilipoichapa AFC Leopards 4-1, nyota wa mchezo alikuwa ni Muivory Coast, Gnamien Yikpe aliyetua Yanga, lakini kwenye gemu yao ya Jumapili kazi yote imeachwa mikononi mwa Mganda, Juma Balinya na wakali wengine walikabidhiwa rungu la kumchapa Ingwe.

Straika wa zamani wa mabingwa hao mara 18, Mghana Francis Afriyie alisema licha ya Yikpe kukosekana na kuwapa presha mashabiki wa Gor, lakini anaamini Balinya na Nicholas Kipkirui wataifanya kazi yao kwa ufasaha Jumapili pale Moi Kasarani.

Rekodi zinaonyesha katika Debi sita za hivi karibuni za timu hizo, Gor imeshinda mara tano na sare ikiwa ni moja, kwani mara ya mwisho kwa Ingwe kushinda ilikuwa Machi 6, 2016.

Afriyie anayekipiga Township Rollers ya Botswana kwa sasa alimshauri Kocha Steven Polack kuwachezesha Kipkirui na Balinya kwa pamoja, kuipa presha ngome ya Leoprads na kuwachapa.

“Hii ni mechi ninaipa ushindi Gor, lakini ni kama KOgalo itachezesha Kipkirui na Balinya pamoja, Ingwe wataumia,” alisema straika huyo Mghana.

Advertisement