BMT yasema ole wao watakaokiuka sheria ya viingilio

Muktasari:

Baraza la Michezo la Taifa msimamizi mkuu wa michezo nchini likifanya kazi zake chini ya mwamvuli wa Wizara ya Habarai, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Dar es Salaam. Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetoa onyo kwa waandaaji wa mashindano yenye viingilio nchini.

BMT imesema waandaaji wa mashindano hayo wanapaswa kulipa asilimia moja ya mapato yatokanayo na viingilio (tiketi) na watakaokiuka hatua kali dhidi yao zitachukulia.

Aidha BMT imewataka pia wadau au wafadhili wanaojitokeza kugharamia viingilio na kuruhusu mashabiki kuingia bure kuhakikisha wanalipa gharama hizo sanjari na kodi.

"Hii ni Sheria ya Baraza kanuni ya 21 (1)," alisema Ofisa habari wa BMT, Najaha Bakari.

Alisema wale waliokwisha endesha mashindano ya viingilio mwaka huu wanapaswa kulipa asilimia moja Baraza kabla hawajachukuliwa hatua.