Ashraf, Zungu kuzichapa Dar es Salaam Jumapili

Thursday November 7 2019

Ashraf- Zungu -kuzichapa -Dar es Salaam- Jumapili-Amour- Zungu -wilaya - Kinondoni-Mabondia - Zanzibar-michezo blog-mwanasport-mwanaspotiGazeti-

 

By Imani Makongoro

Dar es Salaam. Mabondia wa Zanzibar, Ashraf Suleiman na Amour Zungu watapanda ulingoni katika pambano la kuhamasisha ngumi wilaya ya Kinondoni.

Pambano hilo la uzani wa juu litapigwa kwenye ukumbi wa CCM Mwinjuma, Kinondoni likitanguliwa na mengine 10.

Promota wa pambano hilo, Ibrahim Kamwe "Big right" amesema lengo la mapambano hayo ni kurejesha morali ya ngumi Kinondoni.

"Hivi sasa ngumi zinachezwa zaidi Mabibo na Manzese, lakini tunahitaji kurejesha morali hiyo Kinondoni kama ilivyokuwa awali.

Kinondoni ndiko wametokea mabondia, Omari na Said Yazidu, Dullah Mbabe na Francis Miyeyusho ambao walitamba.

Advertisement