Arusha yatakata mashindano ya riadha Taifa

Saturday September 12 2020

 

By Imani Makongoro

Arusha imeanza kwa kishindo mashindano ya Riadha ya Taifa yanayofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya kuvuna medali tano katika fainali ya mbio za mita 5000 na 10000.

Mwanariadha nyota wa timu ya Taifa,  Angelina Tsere aliyekimbia kwa dakika  17:02:78 ndiye amefungua pazia la ushindi kwa kutwaa dhahabu kwenye mbio za mita 5000 za wanawake.

Grace Charles aliyekimbia kwa dakika 17.09.36 na Catheline Lange aliyekimbia kwa dakika 17.09.47 walihitimisha tatu bora.

Kilimanjaro ilipata dhahabu ya kwanza katika mbio za mita 10000 huku fedha na shaba zikienda Arusha.

Josephat Gisemo aliyekimbia kwa dakika 29.44.28 ndiye alikuwa kinara akifuatiwa na

 Fabiano Sulle  aliyekimbia kwa dakika  29.47.26 na

Advertisement

Mathayo Sombi aliyekimbia kwa dakika 29.47.18 walihitimisha tatu bora kwa upande wa wanaume.

Kocha wa Arusha, Andrew Panga alisema huo ni mwanzo na kusisitiza kuwa mkoa wake umejipanga kila mwanariadha kurudi na medali.

 

Advertisement