Allegri naye atajwa Man United

Friday October 16 2020

 

MANCHESTER, ENGLAND. KUNA jambo liaendelea pale Manchester United ambapo kumekuwa na taarifa zinazodai kwamba kocha wa sasa wa Ole Gunnar Solskjaer ana hatihati ya kuondoka ikiwa ataendelea kupata matokeo mabaya ambayo yameanza kuzua mtafaruku makubwa kwa mashabiki.

Miongoni mwa makocha ambao wapo kwenye orodha ya kuchukua mikoba ya Ole ukiachilia mbali Mauricio Pochettino ni kocha wa zamani wa Juventus, Massimiliano Allegri ambaye hajapata timu ya kufundisha tokea mwaka 2019 alipoachana na Juventus.

Man United imekuwa kwenye kiwango kibovu tokea ilipoanza Ligi Kuu msimu huu ambapo mchezo wa kwanza ilipoteza dhidi ya Crystal Palace kwa kipigo cha mabao 3-1, sambamba na kipigo cha mabao 6-1 katika uwanja wao wa nyumabani dhidi ya Tottenham Hotspur.

Katika michezo mitatu ya Ligi Kuu, Ole amefanikiwa kushinda mechi moja dhidi ya Brighton kwa mabao 3-2 katika mchezo ambao Man United ilipata bao la jioni kwa njia ya penati iliyoamuliwa baada ya marudio ya VAR.

Man United imeonekana kuwa kwenye hali mbaya hasa katika safu ya ulinzi ambayo mwaka jana ilitumika zaidi ya Pauni 100 milioni ili kuiboresha ambapo Pauni 80 milioni ilitumika kumnunua Harry Maguire na Pauni 50 milioni kwa ajili ya Aaron Wan-Bissaka.

Kutokana na kiwango hicho kumekuwa na taarifa zinazoeleza Man United inamuhitaji, Mauricio Pochettino lakini suala hili linaingia ugumu kwa kuwa kocha huyo anawindwa na Man City hivyo kutakuwa mvutano mkubwa tofauti na Allegri amekuwa nje ya kazi ya ukocha tokea dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2019 na hakuna klabu inayoonekana kumuhitaji.

Advertisement

Allegri aliwahi kuifundisha AC Milan, ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu, Italia sambamba na Coppa Italia ambalo alishinda mara nne na Supercoppa Italia mara tatu.

Fundi huyu kutoka Italia aliwahi kuingia fainali mbili za Ligi ya Mabingwa, mwaka 2015 dhidi ya Barcelona ambapo alipoteza kwa mabao 3-1 na Real Madrid mwaka 2017 kule Cardiff ambapo alipoteza kwa mabao 4-1 na fainali zote aliingia wakati anaifundisha Juve.

Kocha huyo amewahi kukaririwa akisema anatamani kufundisha soka nje ya Italia jambo ambalo linazidisha tetesi za kuwa anaweza kuja kuwa kocha wa klabu hiyo.

 

Advertisement