Alaaa kumbe! Zidane alimtaka Sadio Mane

Friday August 16 2019

 

IMEBAINIKA Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane alimpigia simu staa wa Liverpool, Sadio Mane akimshawishi nyota huyo wa kimataifa wa Senegal kutua kwa wababe hao wa Santiago Bernabeu katika dirisha kubwa lililofungwa England hivi karibuni.

Inadaiwa Mane alivutika na mpango huo lakini mahitaji makubwa ya Liverpool kipesa pamoja na imani aliyonayo Rais wa Real Madrid, Florentino Perez kwamba ana mawinga wengi iliwafanya Madrid waachane na mpango huo.

Juzi, Mane ambaye aliiwezesha Liverpool kutwaa ubingwa wa Ulaya Mei mwaka huu aliendeleza makali yake wakati alipoifungia Liverpool mabao mawili katika pambano la Super Cup dhidi ya Chelsea na kisha Liverpool kutwaa ubingwa huo kwa matuta.

Mane amekuwa na kiwango kizuri ndani ya kikosi cha Liverpool akimfunika Mohamed Salah msimu uliopita ambaye amefunga mabao mengi ya penalti katika Ligi Kuu tofauti na Msenegal huyo.

Advertisement