VIDEO: Babu Seya: Sikulipwa chocote wimbo wa Sea zaidi ya laki mbili ya kuchukulia vyombo

Wednesday September 18 2019

Babu Sea, Mwanaspoti, Nilipata, laki mbili, wimbo wa Sea, Tanzania, Papii kocha

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam."Vaa vizuri mpenzi wangu upendeze Donge liwashike, Mabusu motomoto, Mimi na wewe mpaka kufa eh Mama eh eh eh......."

Hiki ni kipande alichoimba Nguza Viking kati wimbo wa 'Sea' na kama unajua amelipwa wimbo huo utakuwa hauko sahihi.

Nguza viking amepiga stori na MCL Digital Septemba 10, 2019 Bahari Beach jijini Dar es Salaam, amesema hakuna alichokipata katika wimbo wa Sea zaidi ya kupewa laki mbili ya kuchukulia vyombo vya muziki kupeleka studio.

Amesema, wimbo wa Sea ilikuwa 'Project' ya mwanae Johnson Nguza maarufu Papii Kocha na marehemu Ruge Mutahaba, yeye alikuwa tu mtunzi, hivyo aliitwa na Ruge akapewa laki mbili ya kuchukua vyombo kupelekwa studio.

"Mwanangu kwanza nasikitika sana sababu wengine wako mbele za haki sio vizuri kuwazungumzia, yaani katika nyimbo zangu 'Mapromota' na watayarishaji wa muziki ndio wamechukua 'part' kubwa sisi wengine hakuna tulichokipata wimbo wa Salima na Sea zilikuwa 'project' ya Papii na marehemu Ruge Mutahaba mimi ni mtunzi tu,ila katika wimbo wa Sea mimi Ruge aliniita tu na kunipa laki mbili ya kuchukua vyombo na kupeleka studio na kuwalipa wanamuziki

"Kwakuwa mimi nilikuwa na uwezo kidogo ikabidi nimchukue mpiga gitaa Elombee Kichinja na Papii tukaenda studio tukatengeneza wimbo wa Sea basi, hivi navyokwambia wimbo wa Sea hadi leo  sijapata pesa hata kidogo,yaani unielewe laki mbili ni ya kubebea vyombo na sio malipo ya Sea ndio maana nasema sio vizuri kuzungumzia hili sana wakati mwenye project amefariki inakuwa haina maana tena,na tuseme tu sisi tulipewa nafasi kama ya kujitangaza lakini kwenye kipato hakuna tulichopata

Advertisement

"Nashukuru Serikali Waziri Mwakyembe kutangaza wasanii walipwe nyimbo zao kila wimbo ulipiwe, hapa  kafikiria kitu cha msingi sana ambacho kitatusaidia kupata haki yetu" alisema Babu Sea

Babu Sea amesema, sio tu wimbo wa 'Sea' hajalipwa bali hata wimbo wa 'Salima'ambayo pia ilikuwa Project ya Papii na Ruge na wimbo wa Kadilika Simba.

Aidha Babu Sea aliungana na baadhi ya wanamuziki wanaodai media inashusha muziki wa dansi,japokuwa vipo vyombo vya habari vinasema kutokana na baadhi ya wanamuziki wa dansi kutotoa nyimbo zenye tungo nzuri na za kuhamasisha wadau wa muziki wa dansi ili kuwakubali wanashindwa kutumia nyimbo zao katika media zao kwani media nyingi ziko kibiashara hivyo hawawezi fanya biashara ambayo hailipi hata kwa kuilazimisha.

"Muziki wa dansi umeshushwa na media, na kama tunavyojua muziki ni biashara na biashara yeyete Duniani ni matangazo,sasa media imeachia 'kupromote' muziki wa dansi unapromote muziki mingine, hapo hatuwezi kurudi kama zamani, japo na sisi wanamuziki tunatakiwa tubadirike sio kila siku tunapiga muziki staili ya kina Jojina au karubandika,inabidi tusonge mbele twende na wakati hata kama kama nyimbo hazina tungo nzuri zipigwe tu hivyo hivyo"

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisement