Klopp awashukiwa nyota wake kwa kipigo cha Liverpool

Muktasari:

Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, alisema nafasi nyingi walizopata washambuliaji wake zingeipa Liverpool ushindi katika mchezo huo wa Kundi E.

London, England. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amedai wachezaji wake wanapaswa kujilaumu kwa kukosa ushindi dhidi ya Napoli katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Liverpool ilichezea kichapo cha mabao 2-0 ikiwa ugenini yaliyofungwa na Dries Mertens kwa penalti na Fernando Llorente.

Klopp alisema washambuliaji hakuwacheza kwa nidhamu walipokuwa ndani ya eneo la hatari la Napoli.

Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund, alisema nafasi nyingi walizopata washambuliaji wake zingeipa Liverpool ushindi katika mchezo huo wa Kundi E.

“Tumeshindwa wenyewe hakuna wa kumlaumu, tulipata nafasi nzuri za kufunga, lakini tulishindwa.

“Ilikuwa ni mechi ya wazi kwamba kila timu ilikuwa na nafasi kubwa ya kushinda, lakini umaliziaji wetu haukuwa mzuri,”alisema Klopp.

Pia alisema kocha huyo alidai hakubaliani na penalti ya Napoli akidai haikuwa sahihi.

Klopp alisema ameridhika na kiwango cha wachezaji wake kwasababu walitengeneza nafasi za mabao licha ya kutopata ushindi.

Kocha wa Napoli, Carlo Ancelotti alisema mbinu yake imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mtaliano huyo alisema alitoa maelekezo mabeki kucheza kwa nidhamu na mbinu hiyo ilizaa matunda kwani beki wa kati Kalidou Koulibaly alikuwa nyota wa mchezo.