Salamba atua Namungo FC kwa mkopo

Wednesday August 14 2019

 

By Yohana Challe

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba amefanikiwa kujiunga kwa mkopo na timu yake mpya Namungo FC inayojiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Salamba amejiunga na kikosi hicho kwa mkopo wa mwaka mmoja, lakini alishindwa kujiunga na wenzake kutokana na kwenda Afrika Kusini katika majaribio na sasa amerejea kutokana baada ya kushindwa.

Mwenyekiti wa Namungo FC, Hasani Zidadu alisema walimyakua mchezaji huyo kabla ya dirisha la usajili kufungwa, lakini walimuacha kutokana kuwa na mambo mengine binafsi.

"Kama angefanikiwa huko alikokwenda, basi tusingeweza kumpata, lakini imekuwa heli kwetu kumpata mchezaji huyo," alisema Zidadu.

Aliongeza timu hiyo, inatarajia kushuka uwanjani kesho Alhamisi kucheza na Azam B, kwenye Uwanja wa Chamazi Complex ikiwa ni moja ya kuendelea kukinoa kikosi chao.

Advertisement