Wiki ya Mwananchi, Simba Day zitangaliwe kwa jicho hili

Thursday August 8 2019

Mwanaspoti, Michezo, Mwanasport, Wiki ya Mwananchi, Simba Day zitangaliwe, kwa jicho hili

 

By Yohana Challe

Dar es Salaam.Mwanzo wa wiki hii kulikuwa na shangwe la aina yake katika Jiji la Dar es Salaam hasa mashabiki wa Simba na Yanga waliokuwa wakizishuhudia timu zao zikitawatambulisha mastaa wao waliosajiliwa msimu huu

Yanga ilijitupa uwanjani Jumapili iliyopita ikihitimisha 'Wiki ya Mwananchi' ikicheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya na kutoshana nguvu ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa.

Juzi Jumanne Simba nayo ilihitimisha 'Simba Day' kwa kucheza na Power Dynamos na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 yaliyofungwa na mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Meddie Kagere.

Hata hivyo kuna vitu ambavyo uongozi wa timu hizo unapaswa kuvitazama zaidi ili kuendeleza na kudumisha siku hizo zilizoigusa serikali baada ya kujishughulisha na mambo ya kijamii kama vile kuchangia damu na kufanya usafi kwenye vituo vya afya. Pia mambo haya lazima yatazamwe upya.

IDARA YA MASOKO

Michezo ni ajira kwa vijana wengi, umati uliojitokeza siku hizo ili kujipatia mapato zaidi bado kulionekeana kulegea kwa upande wa masoko kwa timu, mfano kutokuwepo kwa sehemu ya chakula na hata vinywaji.

Advertisement

INSHU YA TIKETI

Mashabiki wengi walilalamikia kupewa tiketi zilizotumika na zilizofanana, jambo ambalo linaweka taswira mbaya kwenye soka letu.

Hata hivyo jambo hilo limeifanya Yanga kulalamikia mapato yaliyopatikana kwenye mchezo wao na kueleza kuchukua hatua kwa wote wanaohusika ili kuhakikisha haki yao inapatikana na kula nao sahani moja kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya Township Rollers wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

UWEZO WA WACHEZAJI

Ilikuwa siku maalum kwa timu hizo kutambulisha wachezaji wao, na ndilo lililotegemewa kwa mashabiki kuwaona mastaa watakaotumia msimu huu wa ligi.

Kila upande kulizungumzwa kulingana na uwezo wa wachezaji waliopata nafasi ya kucheza siku hiyo, wapenzi wa Simba walifurahi kusikia jina la Ibrahim Ajibu pamoja na Gadiel Michael lakini walikoswa na kiwango cha kiungo wao mpya Sharaf Shiboub.

Uwezo wa wachezaji, hamasa, vitu vya kujifunza pamoja na uuzwaji wa jezi kutanatakiwa kutazamwa zaidi njia nyingine maana tayari janja janja zimeonekana kuanza kutumika kwa watu kupiga pesa kwa njia zisizo sahihi.

Advertisement