Kipa Shikalo atua Dar aifuata Yanga Moro

Muktasari:

Ujio wa kipa Farouk Shikalo kunaifanya sasa Yanga kukamilisha idadi kamili ya wachezaji wake wa kigeni.

Dar es Salaam. Kipa mpya wa Yanga wa Mkenya Farouk Shikalo amewasili rasmi nchini kujiunga na timu hiyo kambini Morogoro.

Shikalo amewasili mchana wa leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tayari kuanza maisha na klabu yake ya Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Bandari FC.

Kipa huyo alisema sasa anaangalia mbele kuhakikisha anaifanya kazi yake kwa uwezo mkubwa kuipa mafanikio Yanga.

Shikalo alisema anajua Yanga ni klabu kubwa na sasa yupo tayari kushirikiana na wenzake kuipa mafanikio Yanga.

Ujio wa Shikalo kunaifanya sasa Yanga kukamilisha idadi wachezaji wake wa kigeni.

Yanga sasa idadi ya wachezaji wao 10 wa kigeni watakuwa Shikalo, mabeki Lamine Moro, Mustapha Seleman.

Wengine ni pamoja na washambuliaji Issa Bigirimana, Patricy Sibomana, Juma Balinya na Sadney Urikhob ambao wataungana na Wakongomani wawili waliowakuta kipa Klause Kindoki na kiungo Papy Tshishimbi.