Matizi ya Simba Afrika Kusini lazima ukae

Muktasari:

Katika programu hiyo Kocha Patrick Aussems aliwagawa katika makundi mawili.

Rosternburg.  Moto unaowashwa kwa wachezaji wa Simba hapa Afrika Kusini si wa kitoto ni mazoezi tu leo Jumapili kila mchezaji anafanya ya gym na uwanjani.

Iko hivi, katika programu hiyo Kocha Patrick Aussems aliwagawa katika makundi mawili.

Asubuhi washambuliaji baadhi ya viungo na makipa, walifanya mazoezi ya gym walikuwa chini ya Kocha Adel Zrane.

Mabeki wote pamoja na baadhi ya viungo walikuwa uwanjani na Aussems.

Programu hiyo jioni itabadilika ambapo waliofanya gym asubuhi watakuwa na Aussems uwanjani. Waliofanya uwanjani watakuwa na Adel gym.

Programu ya kesho itaendelea kama kawaida ambapo sasa kocha anachanganya mazoezi ya nguvu, mbinu na ufundi.