Mshambuliaji Martin azipa saluti Simba, Yanga

Monday June 10 2019

 

By OLIPA ASSA

Dar es Salaam. Mshambuliaji Ruvu Shooting, Emmanuel Martin amesema msimu huu kwake ulikuwa wa kujifunza maisha nje ya Yanga na kudai mtazamo wake kwa sasa umekuwa wa tofauti.

Martin alisema mchezaji akiwa ndani ya Simba na Yanga ni ngumu kuona changamoto za upambanaji kwa madai akitoka nje ya hapo ipo thamani ama somo anapata.

"Simba na Yanga ni rahisi kumjulisha mchezani yupo wapi, tofauti na timu nyingine ambazo bila uwezo unapotea machoni mwa mashabiki.

"Nimejifunza kuthamini nafasi ninapokuwa unapewa na kocha pia juhudi binafsi, mfano Salim Aiyee wa Mwadui FC anaonekana thamani yake kwa sababu ya kazi aliyofanya.

"Alikuwa anakimbizana kufunga na wachezaji wa Simba na Yanga, lakini kama huna jambo basi ngumu sana kutoboa, imenijenga kujituma kwa bidii kufikia malengo yangu, natamani kucheza nje," alisema Martin.

Advertisement