Meck kwa tambo sasa

Saturday June 8 2019Kocha wa Kagera Sugar, Meck Maxime

Kocha wa Kagera Sugar, Meck Maxime  

By THOMAS NG'ITU

KOCHA Meck Maxime wa Kagera Sugar ametamba kwamba alikuwa anajua kabisa timu hiyo haiwezi kushuka daraja hata kidogo.

 

Kagera Sugar iliyomaliza Ligi ikiwa na pointi 44 sawa na Mwadui iliwalazimu kucheza Play Off na timu za Ligi daraja la kwanza na bingwa ndio angeendelea kusalia.

 

Mwadui walicheza na Geita mchezo wa kwanza walitoka 0-0 (Geita) huku Pamba na  Kagera nao wakitoka  0-0 na katika mchezo wa marudiano Mwadui waliibuka na ushindi wa 2-1 (Shinyanga) na Kagera Sugar wakiibuka 2-1 (Kaitaba).

 

Advertisement

Baada ya matokeo hayo, Meck alisema alikua anajua sehemu gani ambayo walikosea katika Ligi Kuu hivyo alifanya marekebisho na kuamini kabisa kwamba wanasalia na kutoshuka Ligi Daraja la Kwanza.

 

"Sikuwa na presha yoyote kwasababu sisi ni watu wa Ligi Kuu, lakini nachoweza kusema kwamba wapinzani wetu walitoa ushindani na sisi tumepambana kuhakikisha kwamba tunapata matokeo," alisema.

 

Wakati huo huo kocha wa Pamba, Ally Kisaka alisema mchezo huo walianza kufungwa nje ya uwanja baada ya kupata buguza kutoka kwa mapolisi.

 

"Ndani ya uwanja kweli wenzetu walikuja na kutuzidi lakini tangu tumefika hapa tumekuwa tukisumbuliwa na mapolisi, wachezaji wangu wanasukumwa ovyo tu na polisi kwahiyo walikuwa wameshatoka mchezoni.

 

Magoli ya Kagera Sugar ayalifungwa na Ally Ramadhan dakika 50 huku la pili likifungwa na Japhet Makalai dakika 79.

Advertisement