Mabao ya Bocco, Kagere wampagawisha Mo Dewji

Muktasari:

Katika mchezo huo mabao ya Simba yalifungwa na Bocco mawili, Kagere na Chama kila moja lifunga bao moja

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ameshindwa kujizuia kwa kushangilia kwa nguvu wakati vijana wake wakichapwa mabao 4-5 na Sevilla kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mo Dewji alishinda kujizuia ni baada ya kufungwa bao la tatu na John Bocco aliyepokea pasi kutoka kwa Meddie Kagere.

Mo Dewji aliyekuwa ameketi karibu na Mkurungezi wa Utawala na Udhibiti wa Sportpesa, Abbas Tarimba alianza kushangilia kwa nguvu huku akirukaruka baada ya Simba kupata bao la tatu.

Mo Dewji alikuwa amesimama huku akirukaruka na kumpa mkono wa pongezi Tarimba.

Baada hapo Mo Dewji alikaa chini huku akionekana bado kuwa na furaha akiwapa mkono wa pongezi waliokuwa karibu yake.

Mo Dewji hakushngilia bao hilo peke yake kwa upande wa viongozi waliokuwa hapa jukwaa Kuu ni Mtendaji Mkuu wa Simba, Magori, Mwenyekiti Swedy Mkwabi.

Wengine Hussein Kita, Mulamu Ng'ambi, Mwina Kaduguda wote na Wajumbe wa Bodi, bila kumsahau Ofisa habari wa Simba, Haji Manara aliyekuwa amekaa karibu na wanamitindo Hamisa Mobeto.

Manara baada ya timu yake kufunga bao la 4-2, aliliamsha akiwa jukwaani.

Ilikuwa hivi, bao la nne la Simba lilifungwa na Clatous Chama aliyemalizia pasi nzuri ya John Bocco.

Baada ya kufunga bao hili Mo Dewji kama kawaida aliliamsha kwa kupiga shangwe huku akiwa anaruka ruka.

Manara ndio alilimsha kwani alitoka pale kwenye kiti chake na kwenda mbele ya Jukwaa Kuu walipo wageni walikwa kuanza kucheza.

Manara alikuwa akicheza kama vile mashabiki wa Simba waliokuwa Uwanjani hapo wakishangilia nao la Chama.

Katika kushangilia kwa Manara huku akiwa anacheza alichukua pochi yake ya kihifadhia pesa kana kwamba anataka kutoa kuwarushia mashabiki.

Baada ya muda Manara alionekana kumaliza kucheza nakurudi katika kiti chake akiwa amekaa karibu na Hamisa Mobeto.