Simba, Sevilla FC mechi ya mwisho kwa kocha Caparros

Wednesday May 22 2019

Simba, Sevilla FC, Mwanaspoti, kocha Caparros, Michezo blog, Michezo, Mwanasport

 

By Majuto Omary

Dar es Salaam. Timu ya Sevilla imetangaza kocha wake mkuu Joaquín Caparros atakuwa anakaa katika benchi la ufundi kwa mara ya mwisho katika mchezo wa wake dhidi ya Simba.

Hatua ya kumbadilisha Capparros imetangazwa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini leo jioni.

Mmoja wa viongozi wa timu hiyo alisema kuwa mkutano uliofikia uamuzi uliendeshwa na Rais wa timu hiyo, José Castro. Mkutano huo ulihudhuriwa na meneja wa michezo wa timu hiyo, Monchi.

Kocha huyo atapewa majukumu mengine katika timu hiyo.  Caparrós ameifundisha timu hiyo misimu mitatu.

Caparrós, 64, ameingoza timu hiyo katika mechi 510 za ligi ya La Liga ikiwa, ikiwa mechi 167 akiwa na Sevilla FC.

Pia kocha mwingine, Luci Martín ameondolewa katika benchi la ufundi kwa timu hiyo.

Advertisement

Advertisement