Manchester United hiyooo ‘top four’ EPL

Saturday February 9 2019

 

England. Timu ya Manchester United imetinga kwenye nafasi nne za juu Ligi Kuu England leo Jumamosi baada ya kuifunga Fulham mabao 3-0.

Mabao ya Manchester United yalifungwa na Paul Pogba (14’ na 65’) pamoja na Anthony Martial (23’).

Ushindi huo umeifanya Man United kutinga hadi nafasi ya nne ikiwa na alama 51 na kuongeza  presha ya mbio za ubingwa ikiwa na tofauti ya alama 11 na kinara Manchester City wenye pointi 62.

Kikosi cha Manchester United kilichoanza kilikuwa kinaundwa na; De Gea, Dalot, Smalling, Jones, Shaw, Ander Herrera, Matic, Pogba, Mata, Lukaku, Martial, huku benchi kukiwa na kina Bailly, Sanchez, Rashford, Lingard, Young, Romero, McTominay

 

Advertisement