Liverpool yaisambaratisha Man United ya Mourinho

Muktasari:

Manchester United sasa wameruhusu mabao 29, moja zaidi waliyofungwa katika msimu mzima wa 2017/18 walipofungwa mabao (28).

London, England. Xherdan Shaqiri aliingia akitokea benchi na kufunga mabao katika ushindi wa Liverpool wa magoli 3-2 dhidi ya Manchester United na kurudi kileleni mwa Ligi Kuu England.

Liverpool ilihitaji kushinda baada ya Manchester City kuichapa Everton jana Jumamosi, ilikuwa ni siku njema kwa Shaqiri aliyeingia akitokea benchi katika kipindi cha pili aliyemwakikishia Jurgen Klopp pointi tatu muhimu.

Sadio Mane alifunga bao kwanza dakika 24, akiunganisha pasi ya Fabinho, lakini ushindi huo ulidumu kwa muda mfupi baada ya makossa ya kipa Alisson aliipa Man United bao la kusawazisha wakati krosi ya Romelu Lukaku ilipompita na kumkuta Jesse Lingard aliyefunga bao la kusawazisha.

Man United ilijaribu kufanya mashambulizi, lakini Liverpool ilibadilika baada ya Klopp kumwingiza Shaqiri zikiwa zimebakia dakika 20, na kubadilisha upepo.

 Shaqiri alifunga bao lake la kwanza kwa shuti lilomgonga Ashley Young na kumpotea kipa David de Gea, lakini Shaqiri alifunga bao pili kwa shuti lake tena kumgonga beki Eric Bailly na kumpita de Gea na kuwahakikishia wenyeji Liverpool ushindi mnono wa mabao 3-1.