Ramani ya ubingwa wa Simba ulikuwa hivi

SIMBA imechukua taji lao na walistahili kulichukua kwa vita ambayo walipigana ndani ya uwanja na hata nje ya uwanja. Wamechukua taji lao la tatu mfululizo la Ligi Kuu Bara baada ya jana kumalizana na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Safari ya Simba kuchukua ubingwa ilikuwa na sura tofauti ambapo hapa Mwanaspoti inakuletea jinsi wekundu hao walivyolichukua taji hilo kibabe.

Ushindi wa kwanza ligi 3-1

Simba ilianza ligi Agosti 29,2019 mchezo ukisomeka akiwa mgeni mbele ya JKT Tanzania na wakataka wakiwachapa wanajeshi hao kwa mabao 3-1, shukrani kwa mabao mshambulaiji wao Meddie Kagere aliyefunga mara mbili katika mchezo huo dakika za 1 na 59 kisha bao la ushindi likifungwa na Miraji Athuman 73 huku Edward Songo akiifungia timu yake bao la kufutia machozi dakika ya 87.

Ushindi huu ulikuwa na maana kubwa kwa Simba wakati huo ikiwa chini ya kocha Patrick Aussems kufuatia walitoka kupokea taarifa mbaya wakitupwa nje ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji wakiwa hawakutarajia.

Ushindi mkubwa mabao 8

Simba ushindi wake mkubwa mpaka jana inachukua ubingwa ni ule walioichapa Singida United kwa mabao 8-0, walima alizeti kutoka kule mkoani Singida kipigo hicho hawatakisahau wakati wakielekea kucheza ligi daraja la kwanza msimu ujao ambapo, hawakuwa na hoja siku hiyo walipokutana na wekundu hao.

Mbali na ushindi huo Simba pia ilikuwa inagawa dozi zingine kali wakishinda kwa mabao 4 katika mechi tatu tofauti wakifanya hivyo nyumbani dhidi ya Mbeya City kisha Lipuli ya Iringa na baadaye walifanya hivyo tea mbele ya Alliance ya Mwanza ugenini.

Walipigwa hivi

Simba ilipoteza mara tatu katika ubingwa wao huu wakianza kupoteza mara ya kwanza dhidi ya Mwadui ya Shinyanga (1-0) kocha akiwa Aussems kisha baadaye wakaumia dhidi ya Ruvu Shooting kwa kipigo kama cha kwanza.

Kipigo cha pili ambacho kiliwaumiza Wekundu hao ni pale walipopoteza mbelea ya watano zao wa jadi, Yanga kwa bao pekee la mshambuliaji Bernard Morrison, kifupi kila mchezo alipoteza kwa bao moja tu.

Sare tatu msimu mzima

Mpaka taji linakamilika Simba imetoa sare tatu pekee na zote akiwa nyumbani akianza na Prisons wakitoka suluhu, ya pili ilikuwa ni dhidi ya Yanga mchezo ukimalizika kwa mabao 2-2 na mchezo wa tatu ukawa ni dhidi ya Ruvu Shooting wakifungana bao 1-1.

hakuachi nyumbani, hakuachi ugenini

Simba alikuwa hachagui wapi kwa kutoa kipigo uwe nyumbani wala ugenini, kwani alishinda mechi 13 nyumbani ikiwa ndio timu iliyoshinda mechi nyingi nyumbani lakini pia wakashinda 12 ugenini ambako walikotangazia ubingwa msimu huu.

Makocha wawili msimu mmoja

Ubingwa huu wa tatu mfululizo Simba imeuchukua ikiwa na makocha wawili tofauti wakianza msimu na Aussems, ambaye baadaye akasitishiwa mkataba na baadaye kijiti kikachukuliwa na Sven Vandenbroeck jambo zuri ni kwamba, wote walikuwa kutoka taifa moja la Kibelgiji.

Yanga pekee alimkatalia

Timu moja tu msimu huu imefanikiwa kutoka salama mbele ya Simba ambayo ni Yanga, watani hawakukubali kupokea kipigo, Simba alifanikiwa kuambulia pointi moja tu na baadaye wakapoteza mbelea ya Yanga mpaka wakati huu wanatangaza ubingwa.