Prince Harry sasa ni baba

Friday May 10 2019

 

By Elizaberth Edwald

ACHANA na zile vurugu zake, kwa sasa Prince Harry amekuwa mtu mzima na ameacha vituko vya kuruka ukuta, kutoroka walinzi wake na kwenda kula bata klabu za starehe usiku mwingi.

Juzi Prince Harry na mkewe Meghan Markle wamepokea mgeni mpya duniani, ambaye akiwa na siku chache tu tayari dunia imetikisika na vyombo vya habari kumuangazia.

Awali, ilielezwa kuwa Meghan alikuwa kwenye hatua za mwisho za kujifungua na sasa mgeni huyo ameshatua na kuwa gumzo kila kona huku kwenye familia ya Malkia Elizabeth kuwa ni shangwe tupu.

Lakini, juzi wanandoa hao wakaweka hadharani furaha yao kwa kutangaza kupata mtoto wa kiume aliyepewa jina la Archie.

Picha ya kwanza iliwaonyesha Meghan na Harry wakiwa wamembeba Archie muda mfupi tu baada ya kutoka hospitalini.

Advertisement