Masikini! Chamberlain ndiyo basi tena

Thursday July 19 2018

 

London, England. Alex Oxlade-Chamberlain uenda akaukosa msimu wote ujao baada ya kufanyiwa vipimo upya vya goti lake kwa mujibu wa ripoti iliyotoka jana Jumatano.

Kiungo huyo wa Liverpool mwenye miaka 24, alivunjika zaidi ya mara moja goti lake wakati wa mchezo wa kwanza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma iliyochezwa Aprili.

Kila mfupa wake wa goti la kulia uliumia pamoja na mishipa ya cruciate, medial na lateral collateral ligaments.

Kiungo huyo wa kimataifa wa England aliyekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Jurgen Klopp pia aliumia tendon iliyosababisha kuwa na tatizo la nyonga la muda mrefu.

Kutokana na hali hiyo anatakiw akufanyiwa upasuaji mwingine katika siku nane zijazo chini ya uangalizi wa mtaalamu wa upasuji wa goti Dk Andy Williams hivyo kuna uwezekano Oxlade-Chamberlain anaweza kurudi uwanjani Novemba.

Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa Oxlade-Chamberlain zinasema mchezaji huyo ameambiwa ili aweze kurudi katika kiwango chake za zamani anatakiwa kukaa nje ya uwanja wa miezi 12.

 

Advertisement