Chege: Muziki wa sasa mzuri, ubunifu uongezeke

Tuesday September 10 2019

 

By Olipa Assa

Dar es Salaam. Msanii wa bongo fleva, Chege Chigunda ameshauri muzikiki wa sasa kuongeza ubunifu utakaoendana na sayansi na tekinolojia ili ushindani uwe mkubwa zaidi.
Chege amesema wasanii wa sasa wapo vizuri kwenye kazi zao kwamba zinaendana na dunia ilivyo isipokuwa ameona ubunifu nikitu kinachokosekana kwao.
"Nawakubari wasanii wote, wanafanya kazi nzuri lakini waongezee ubunifu ambao utafanya nyimbo zao ziwe bora zaidi ya kile wanachokifanya kwa sasa"
"Muziki ni kazi naamini kila msanii, anaipenda hivyo lazima uthamani wao uwe kwenye maishairi yao wanayoyapeleka kwa jamii, inayowaunga mkono"
"Zamani wakati sisi tunaanza kufanya muziki ilikuwa burudani zaidi ila kwa sasa ni biashara na ndio maana unaona ushindani mkubwa kila mtu anataka kusikika, wasikike ila ubunifu uwe mkubwa zaidi"anasema.

Advertisement