Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zlatan kuanzia miaka 30, mabao 250

Muktasari:

Zlatan alifunga bao hilo la kuongoza katika dakika ya 30 ya pambano na kwa kufanya hiyo hilo lilikuwa bao lake la 250 tangu atimize umri wa miaka 30 na hivyo, kumfanya awe mchezaji veteran aliyefunga zaidi katika soka.

SIJUI Zlatan Ibrahimovic atazeeka lini. Rekodi zinaonyesha kuwa kadri anavyozeeka ndivyo anavyokuwa mtamu zaidi. Juzi amefunga bao dhidi ya Sunderland katika ushindi wa mabao 3-0 ugenini na bao lake hilo limekuja na rekodi ya aina yake.

Zlatan alifunga bao hilo la kuongoza katika dakika ya 30 ya pambano na kwa kufanya hiyo hilo lilikuwa bao lake la 250 tangu atimize umri wa miaka 30 na hivyo, kumfanya awe mchezaji veteran aliyefunga zaidi katika soka.

Rekodi hiyo ipo kwa soka la ngazi zote ingawa Zlatan (35), ameendelea kufunga zaidi katika soka la England ambalo linachezwa kwa ushindani mkubwa. Alifikisha umri wa miaka 30 katika msimu wa 2010-11 wakati akikipiga na AC Milan kwa mkopo akitokea Barcelona ambako, alishindwa kuelewana na kocha, Pep Guardiola.

Kuanzia umri huo wa miaka 30, Zlatan alikipiga katika klabu ya Milan kwa uhamisho wa kudumu kuanzia mwaka 2011 mpaka 2012. Baada ya hapo alihamia PSG alikocheza kwa misimu minne kuanzia mwaka 2012 mpaka 2016.

Mwenyewe amekiri kwamba anaendelea kuzeeka na utamu wake kutokana na kufanya mazoezi ya nguvu.

“Nafanya mazoezi ya nguvu, vile vile naendelea kuwa makini. Naamini katika ninachokifanya. Najiamini mwenyewe na kile ninachoweza kukifanya uwanjani na sina wasiwasi nacheza mechi yangu na ninafurahia,” alisema Zlatan.

“Nina wasiwasi kuwa kadri ninavyozeeka ndivyo ninavyokuwa na akili zaidi. Ni kweli kwamba siwezi kuwa na kasi kama ya miaka 10 au mitano iliyopita, lakini kadri ninavyokuwa mzee ndivyo ninavyokuwa na akili na uzoefu zaidi. Hauhitaji kupoteza nguvu nyingi katika vitu ambavyo hauvihitaji. Nilizaliwa mzee na nitakufa kijana,” aliongeza Zlatan.

Mlinzi wa zamani wa Manchester United, Phil Neville, ambaye kwa sasa ni mchambuzi maarufu wa soka nchini England, amedai kwamba msimu huu Zlatan ameibeba Manchester United peke yake katika mabega yake na United watalazimika kumbakiza kwa ajili ya msimu ujao.

“Ameibeba timu yeye mwenyewe, mabao ambayo amefunga, tabia yake uwanjani, Jose anaendelea kubadilisha kikosi lakini kamwe hajawahi kumbadilisha Zlatan, ambaye amecheza dakika zote kila mechi,” alisema Neville.

“Na United watahitaji aendelee kufunga mabao kuanzia sasa hivi mpaka mwishoni mwa msimu. Bao alilofunga (juzi) lilikuwa zuri sana ingawa kulikuwa na makosa ya ulinzi kutoka kwa (Lamine) Kone,” aliongeza Neville.

Kabla ya rekodi ya juzi, tayari Zlatan alikuwa ameweka rekodi mbalimbali Manchester United na katika Ligi Kuu ya England ikiwa ni msimu wake wa kwanza tu Old Trafford na katika Ligi hiyo.

Awali, Zlatan alikuwa mchezaji wa nne wa Manchester United kufikia mabao 15 ndani ya mechi 23 tu tangu akipige klabuni hapo. Wachezaji wanaoshikilia rekodi hiyo mbele yake ni Ruud Van Nistelrooy aliyetumia mechi 19, Dwight Yorke aliyetumia mechi 20 pamoja na Robin van Persie aliyetumia mechi 21.

Zlatan pia alikuwa mchezaji wa kwanza wa Manchester United kufunga katika mechi tatu mfululizo za kwanza za Ligi. Mchezaji wa mwisho kufanya hivyo alikuwa ni Ian Storey-Moore msimu wa 1971-72. Lakini, msimu huu Zlatan amefunga mabao 20 na zaidi kwa msimu wake wa 10 mfululizo katika Ligi mbalimbali alizocheza. Mara ya mwisho kwake kushindwa kufikia mabao 20 ilikuwa ni katika msimu wa 2006-07 akiwa na Inter Milan ambapo alifunga mabao 15 tu.

Pia, kwa kufunga katika pambano la kwanza la Ligi Kuu msimu huu dhidi ya Bournemouth, Zlatan alikuwa ameweka rekodi ya kufunga katika mechi yake ya kwanza akijiunga na klabu baada ya kufanya hivyo na Serie A, La Liga, Ligue 1 na pambano lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa.