Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rweyemamu afichua kilichoipa Yanga mataji mfululizo


MENEJA wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema sababu ya Yanga kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara nne mfululizo, haikuwa bahati mbaya, bali mafanikio hayo yalijengwa kwa misingi ya wachezaji wazawa wenye viwango vikubwa.


Akizungumza wakati wa mahojiano yake na Mwanaspoti, Rweyemamu aliifafanua kauli yake, ili timu iweze kufanya vizuri licha ya uwepo wa maproo bora, lazima iwe na mastaa wazawa waliyo na ubora wa hali ya juu, akiamini hicho ndicho kilichoifanikisha Yanga ndani ya muda huo kuchukua mataji baki tu baki.

Alitolea mfano wa msimu wa 2011/12  baada ya Simba kunyakua ubingwa, ilipita  takribani miaka mitano bila taji hilo ambapo Azam FC ikachukua 2013/2014 kutokana na kuwa na kikosi bora, miongoni wa wachezaji waliyokuwepo  golini alikuwa Aishi Manula, Kipre Tchetche, John Bocco, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure’, Said Morad, Aggrey Morris, Erasto Nyoni na Gaudence Mwaikimba.

“Ukiangalia kikosi cha Azam wakati huo kilichoisaidia kunyakua ubingwa asilimia kubwa wazawa walikuwa na viwango vya juu, iliyosaidiana na ya wageni ambao walikuwa na uwezo mkubwa, vivyo hivyo kwa Yanga kulikuwa ina Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, ukuta huo ndio ulikuwa unatumika mara nyingi katika majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania,” alisema meneja huyo na kuongeza;

“Kabla ya Clement Mzize kuumia alikuwa katika upepo wa kufunga mabao msimu uliyopita alikuwa na mabao 14, asiti tano wa nyuma yake alifunga mabao sita na asisti saba, unaweza ukaona kikosi cha wazawa kilikuwa bora, sasa waliongezeka na wageni kama Fiston Mayele, Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli, ukiachana na kelele za mitandaoni mpira wa miguu unahitaji uwekezaji wa wachezaji bora.”

Alisema wakati Simba ilipoanza kupindua meza ya kuchukua ubingwa wa baki tu baki kuanzia msimu wa 2017/18 hadi 2020/21 ilikuwa wazawa wa viwango vya juu waliyoleta mapinduzi ambao ni Manula, Nyoni, Shomari Kapombe na Bocco waliyosajiliwa kwa pamoja kutoka Azam.