Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zlatan atia tiki usajili wa Rashford Milan

Muktasari:

  • Rashford amekuwa akisakwa na klabu kibao za Ulaya baada ya mwezi uliopita kudai kwamba yupo tayari kuachana na Manchester United kwenda kukabiliana na changamoto mpya.

MILAN, ITALIA: MIAMBA ya soka ya Italia, AC Milan inatarajia kukoleza mwendo kwenye mpango wa kunasa saini ya mshambuliaji Marcus Rashford ndani ya mwezi huu, huku staa wa zamani wa kikosi hicho cha Serie A, Zlatan Ibrahimovic akiunga mkono usajili huo.

Rashford amekuwa akisakwa na klabu kibao za Ulaya baada ya mwezi uliopita kudai kwamba yupo tayari kuachana na Manchester United kwenda kukabiliana na changamoto mpya.

Kwa mujibu wa gazeti la Calciomercato, Ibrahimovic, ambaye kwa sasa ni mmoja wa mabosi huko Milan, anaamini mchezaji mwenzake huyo wa zamani wa Man United waliyecheza pamoja Old Trafford atakwenda kupata mafanikio makubwa San Siro.

Man United haipo tayari kumruhusu Rashford kwenda kujiunga na klabu nyingine ya Ligi Kuu England ikiwa na hofu ya kuimaarisha timu inzani, hivyo ishu ya kwenda Serie A inapewa kipaumbele kikubwa.

Lakini, shida inakuja kwenye mshahara wa mchezaji huyo, ambapo kwa sasa Rashford analipwa zaidi ya Pauni 300,000 kwa wiki, ikiwa ni zaidi ya asilimia 50 ya kiwango cha mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Serie A, straika wa Juventus, Dusan Vlahovic. Juventus yenyewe imeachana na mpango wa kumchukua Rashford na sasa miamba hiyo ya Turin inafikiria kupeleka ofa kwa mchezaji mwingine wa Man United, Joshua Zirkzee. Rashford anaripotiwa kuwa kwenye rada za Paris Saint-Germain pia inayodaiwa kuhitaji saini yake. Hata hivyo, AC Milan ndiyo inayoonekana kuwa na nafasi kubwa katika mchakamchaka huo wa kumnasa Rashford, huku ikishika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Serie A huku ikiwa na mechi moja mkokoni, lakini imeachwa pointi 17 na Napoli.

Kikosi cha Milan kimejaa mastaa kibao waliowahi kukipiga kwenye Ligi Kuu England akiwamo Ruben Loftus-Cheek, Fikayo Tomori, Tammy Abraham, Alvaro Morata na Christian Pulisic.