Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Xavi Simons aona mwezi Tottenham Hotspur

XAVI Pict

Muktasari:

  • Guglielmo Vicario aliokoa hatari muhimu mapema, kabla ya Spurs kufungua bao kupitia kwa Richarlison dakika ya 25 akiunganisha pasi ya Xavi Simons.

LONDON, ENGLAND: ALIYEWAHI kuwa kocha wa Brentford, Thomas Frank, alipata ushindi dhidi ya klabu yake ya zamani baada ya Tottenham Hotspur kukatiza mwendo wa mechi tano bila ushindi kwa kuchukua pointi tatu muhimu kwa ushindi wa 2-0, huku Xavi Simons akifunga bao lake la kwanza tangu ajiunge na Spurs.

Guglielmo Vicario aliokoa hatari muhimu mapema, kabla ya Spurs kufungua bao kupitia kwa Richarlison dakika ya 25 akiunganisha pasi ya Xavi Simons.

Simons alifunga bao la pili kwa mbwembwe akichukua mpira eneo lake na kukimbia nalo hadi ndani ya boksi kabla ya kupiga shuti lililoenda chini ya mikono ya Kelleher.

Tottenham nusura waongeze zaidi, huku Brentford wakinyimwa bao la Mohammed Kudus kwa ofsaidi.

Brentford walishindwa kupata mwanya, na makosa ya mwisho ya Thiago yakiweka muhuri wa kukosa pointi tena.

Spurs wanapanda hadi nafasi ya nane, huku Brentford wakishuka hadi ya 14 baada ya kupoteza mechi yao ya nne ugenini.