Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha Spurs awageuzia kibao mashabiki

SPURS Pict

Muktasari:

  • Vicario alifanya kosa karibu na mstari wa pembeni na kumruhusu Harry Wilson kufunga bao katika lango tupu na kuiweka Fulham mbele kwa mabao 2-0 ndani ya dakika sita tu tangu kuanza kwa mchezo wao uliopigwa wikiendi.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Tottenham, Thomas Frank amegeukia mashabiki wa timu hiyo na kuwachana kwa tukio lao la kumzomea kipa Guglielmo Vicario wakati wa mechi yao dhidi ya Fulham.

Vicario alifanya kosa karibu na mstari wa pembeni na kumruhusu Harry Wilson kufunga bao katika lango tupu na kuiweka Fulham mbele kwa mabao 2-0 ndani ya dakika sita tu tangu kuanza kwa mchezo wao uliopigwa wikiendi.

Makosa hayo yalisababisha Spurs kupoteza mechi kwa mabao 2-1 na ikawa ni mechi yao ya nne kupoteza kati ya saba ilizocheza nyumbani katika Ligi Kuu England msimu huu.

Akizungumza kuhusu mashabiki waliokuwa wakimzomea kipa Vicario, kocha Frank amesema: "Sikupenda kuona mashabiki wetu wakimzomea Vic mara baada ya tukio lile na hata mara kadhaa alipogusa mpira.

"Hawawezi kuwa mashabiki wa kweli wa Tottenham; kila mtu anapaswa kumuunga mkono mwenzake, hivyo inatakiwa tuwaunge mkono wachezaji pale wanapokuwa uwanjani. Au kama walishindwa kabisa kuvumilia, wangezomea hata baada ya mechi kumalizika, lakini sio wakati mechi inaendelea, hilo halikubaliki."

"Ukishakuwa nyuma kwa mabao 2-0 baada ya dakika sita, unakuwa na mlima mrefu wa kupanda na unapokuwa kwenye wakati mgumu, kila kitu kinaonekana kwenda kinyume. Baada ya kuruhusu mabao hayo, tulijaribu kucheza kwa haraka kupita kiasi katika kipindi cha kwanza. Tulitaka kurudi mchezoni, lakini hatukuweza kufanya hivyo kwenye kipindi cha kwanza na tukawa bora zaidi kipindi cha pili. Tulipata nguvu kidogo, tukatengeneza nafasi zaidi, lakini hatukuweza kupata bao la kusawazisha."

Hata hivyo, Frank alifurahishwa zaidi na namna wachezaji wake walivyocheza katika kipindi cha pili kiasi cha kupata bao.