Wote vyuma chagua wewe

LONDON, ENGLAND. DIRISHA la uhamisho wa wachezaji la Januari 2023 limeshafungwa na aliyenaswa kanaswa na aliyebaki kabaki.

Lakini, kwenye dirisha hilo la Januari kuna klabu nyingi zilishindwa kufanya biashara ya wachezaji wao waliokuwa ndani ya miezi sita ya mikataba yao na kuhatarisha uwezekano wa kuondoka bure kabisa mwishoni mwa msimu huu kama hawatakuwa wamesaini mikataba mpya katika klabu hizo wanazozitumikia.

Na kinachovutia zaidi ni kwamba mastaa wanaokwenda kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu, wote ni masupastaa wa nguvu, ambao ukinasa huduma zao wataleta kitu kikubwa sana kwenye kikosi chako.

Utasha ngaa, lakini ndiyo hi, hii hapa orodha ya mastaa wa viwango vya dunia ambao mikataba yao inamalizika Juni mwaka huu na watakuwa huru kujiunga na timu yoyote, ujanja ni kuchangamkia tu saini zao.

Hii hapa orodha ya mastaa ambao watapatikana bure kabisa mwishoni mwa msimu huu katika Ligi Kuu tano Bora za Ulaya.


Ligi Kuu England; Youri Tielemans (Leicester), Wilfried Zaha (Crystal Palace), N’Golo Kante (Chelsea), Roberto Firmino (Liverpool), Ilkay Gundogan (Man City), Caglar Soyuncu (Leicester), Naby Keita (Liverpool), Nelson Semedo (Wolves),

Lucas Moura (Tottenham), Yerry Mina (Everton), David de Gea (Man United), Adama Traore (Wolves),

Jesse Lingard (Nottingham Forest), Manuel Lanzini (West Ham), Alex Oxlade-Chamberlain (Liverpool), Vladimir Coufal (West Ham), Reiss Nelson (Arsenal), Diego Costa (Wolves), Willian (Fulham), Axel Tuanzebe (Man United).


La Liga; Karim Benzema (Real Madrid), Marco Asensio (Real Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Inigo Martinez (Athletic Bilbao), Matt Doherty (Atletico Madrid), Luka Modric (Real Madrid), Dani Ceballos (Real Madrid), Nacho Fernandez (Real Madrid), Sergio Busquets (Barcelona), David Silva (Real Sociedad), Mariano Diaz (Real Madrid) na Raul Albiol (Villarreal).


Serie A; Milan Skriniar (Inter), Adrien Rabiot (Juventus), Andrea Belotti (Roma), Stefan de Vrij (Inter), Luis Muriel (Atalanta), Angel Di Maria (Juventus), Chris Smalling (Roma), Roberto Gagliardini (Inter), Juan Cuadrado (Juventus), Alex Sandro (Juventus), Edin Dzeko (Inter), Samir Handanovic (Inter), Olivier Giroud (Milan) na Nemanja Matic (Roma),

Stephan El Shaarawy (Roma), Roberto Pereyra (Udinese), Zlatan Ibrahimovic (Milan), Danilo D’Ambrosio (Inter), Juan Jesus (Napoli) na Pedro (Lazio)


Bundesliga; Marcus Thuram (Gladbach), Evan NíDicka (Frankfurt), Daichi Kamada (Eintracht Frankfurt), Konrad Laimer (Leipzig), Remy Bensebaini (Borussia Monchengladbach), Raphael Guerreiro (Borussia Dortmund), Mahmoud Dahoud (Borussia Dortmund), Marco Reus (Borussia Dortmund) na Mats Hummels (Borussia Dortmund)


Ligue 1; Lionel Messi (PSG), Houssem Aouar (Lyon), Jonathan Bamba (Lille), Moussa Dembele (Lyon), Ross Barkley (Nice), Sergio Ramos (PSG), Alexis Sanchez (Marseille), Sead Kolasinac (Marseille), Aaron Ramsey (Nice),

Wahbi Khazri (Montpellier), Jerome Boateng (Lyon) na Kevin Gameiro (Strasbourg).