Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England yaitupa nje DR Congo, Kane akitupia mawili

Muktasari:

  • England ilipindua matokeo  kipindi cha pili ikitumia dakika 11 kujihakikishia hatua hiyo, baada ya DR Congo kuongoza kipindi cha kwanza.

TIMU ya taifa ya England imetinga hatua ya 16 bora baada ya kuichapa DR Congo mabao 2-1, katika mechi ya hatua ya 32 bora ya Fainali za Kombe la Dunia.

England ilipindua matokeo  kipindi cha pili ikitumia dakika 11 kujihakikishia hatua hiyo, baada ya DR Congo kuongoza kipindi cha kwanza.

Bao la DR Congo lilifungwa dakika ya saba na Brian Cipenga, 28, anayekipiga klabu ya Almeria ya Hispania na kucheza kwa kujiamini zaidi kwa nidhamu na kulinda kwa umakini kuzuia hatari za mashambulizi ya England.

Dakika 45 za kipindi cha kwanza England ilipiga jumla ya mashuti manane, huku manne yakilenga goli, ikipiga pasi 277 zilizofika 253, sawa na asilimia 91, kona mbili na umiliki wa mpira wa asilimia 59.

Kwa upande wa DR Congo inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya pili tangu mara ya kwanza mwaka 1974, kipindi cha kwanza ilimiliki mpira kwa asilimia 41, ikipiga mashuti matatu, huku moja likilenga goli, pasi 198 na zilizofika 170 sawa na asilimia 86.

Kipa wa DR Congo, Lionel Mpasi anayeichezea Le Havye ya Ufaransa anayocheza Mtanzania, Mbwana Ally Samatta alikoa hatari nne zilizokuwa zimelenga goli kipindi cha kwanza.

Mshambuliaji wa England, Harry Kane anayekipiga Bayern Munich, alifunga bao la kusawazisha dakika 75 kwa kichwa na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa timu hiyo.

Dakika 11 baadaye Kane alifunga bao la pili dakika ya 86 kwa shuti kali na kuendelea kuamsha shangwe kwa mashabiki wa England.

Safari ya England kutinga hatua ya 32 bora ilianza kwa kushinda dhidi ya Croatia mabao  4-2,

Ikatoka suluhu 0-0 na Ghana  na kuifunga mabao 2-0 Panama.

Kwa upande wa DR Congo safari yake ya  ilianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ureno, ikafungwa bao 1-0 dhidi ya Colombia na kushinda 3-1 dhidi ya Uzbekistan, huku aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele akiifungia timu hiyo bao moja.