Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

West Ham yawatema 10

Muktasari:

  • Klabu hiyo inakabiliwa na kipindi kigumu baada ya kushuka daraja na inalenga kupunguza gharama pamoja na kujenga kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao. Hata hivyo, haitapata ada yoyote ya usajili kwa baadhi ya wachezaji wanaoondoka bure, akiwemo nyota wa zamani wa Hispania, Adama Traore.

LONDON, ENGLAND. WEST Ham United imetangaza kuachana na wachezaji 10 kufuatia kushuka daraja kutoka Ligi Kuu ya England kwenda Championship.

Klabu hiyo inakabiliwa na kipindi kigumu baada ya kushuka daraja na inalenga kupunguza gharama pamoja na kujenga kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao. Hata hivyo, haitapata ada yoyote ya usajili kwa baadhi ya wachezaji wanaoondoka bure, akiwemo nyota wa zamani wa Hispania, Adama Traore.

Traore alijiunga na West Ham mwezi Januari akitokea Fulham kwa mkataba wa muda mfupi uliomalizika mwishoni mwa msimu. Mara nyingi alitumika kama mchezaji wa akiba, lakini mchango wake haukuweza kuisaidia timu kuepuka kushuka daraja.

Miongoni mwa wanaoondoka pia ni kipa mkongwe Lukasz Fabianski alikuwa aondoka mwishoni mwa msimu uliopita, lakini akarudishwa miezi michache baadaye kama chaguo la tatu golini baada ya kuondoka kwa Wes Foderingham.

Kipa huyo wa zamani wa Arsenal alijiunga na West Ham kutoka Swansea City mwaka 2018 na kucheza zaidi ya mechi 215 katika kipindi chake cha miaka minane klabuni hapo, akishindania nafasi na Alphonse Areola katika misimu ya hivi karibuni.

Pia, Axel Disasi ataondoka na kurejea Chelsea baada ya kumalizika kwa mkopo wake. Alijiunga Januari na haraka akawa sehemu muhimu ya safu ya ulinzi chini ya kocha Nuno Espirito Santo pamoja na Konstantinos Mavropanos.


WACHEZAJI WA AKADEMI WANAOONDOKA NI:

Michael Forbes,Junior Robinson,Tyron Akpata, Daniel Rigge, David Chigwada,Tom Wooster na Jonathan Unwin.

Michael Forbes ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ireland Kaskazini, hatoongeza muda wake wa miaka sita katika mfumo wa vijana wa West Ham. Naye Junior Robinson ametumia msimu uliopita kwa mkopo katika Boreham Wood.

West Ham sasa inatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi katika jitihada za kurejea haraka kwenye Ligi Kuu.