Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wembanyama anadaiwa kukaribia futi nane

WAMBENYANA Pict

Muktasari:

  • Awali, timu yake ya San Antonio Spurs inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ilimuorodhesha kuwa na urefu wa futi 7 na inchi 3, ingawa mashabiki wamekuwa wakidai muda mrefu kuwa ni mrefu zaidi.

TEXAS, MAREKANI: YULE fundi wa mpira wa kikapu wa kimataifa wa Ufaransa, Victor Wembanyama anadaiwa kuongezeka kwa nchi nne na sasa ikielezwa kwamba kuwa anakaribia urefu wa futi nane.

Awali, timu yake ya San Antonio Spurs inayoshiriki Ligi ya Kikapu Marekani (NBA) ilimuorodhesha kuwa na urefu wa futi 7 na inchi 3, ingawa mashabiki wamekuwa wakidai muda mrefu kuwa ni mrefu zaidi.

Katika taarifa mpya kwenye tovuti rasmi, Spurs imemweka Wembanyama akiwa na urefu wa futi 7 na inchi 5 na uzito wa kilo 106.5, jambo linalomfanya kuwa mchezaji mrefu zaidi NBA.

Wachambuzi wa NBA na wachezaji wa zamani wanasema mchezaji huyo ambaye kifupi huitwa Wemby anaweza kuwa na futi 7 na inchi 7 kwa sasa na ni suala la muda tu kabla hajafikia nane, kwani kwa umri wake wa miaka 21 lolote linaweza kutokea ikizingatiwa kwamba ameongezeka inchi karibu sita tofauti na misimu mitatu iliyopita alipochaguliwa kwenye draft ya NBA.

Mchezaji wa zamani wa NBA raia wa Serbia, Boban Marjanovic ambaye alikuwa na futi 7 na inchi 4 wakati wa maisha yake ya uchezaji, alisema ilibidi awe amwangalia Wemby kwa juu kila alipokutana naye uso kwa uso uwanjani.

“Nina urefu rasmi wa futi 7 na inchi 4, nilipomtazama (Wemby) nilijua kabisa haiwezekani niwe mrefu kuliko yeye,” Marjanovic aliambia SportsCenter.

Naye mchambuzi wa muda mrefu wa NBA, Brian Windhorst, aliongeza: “(Wemby) aliorodheshwa kuwa na futi 7 na inchi 3 akiwa mchezaji chipukizi, lakini hiyo haikuwa kweli. Sidhani kama ilikuwa sahihi naamini ana takriban futi 7 na inchi 5. Ila naamini anaweza kuwa anakaribia futi 7 na inchi 7.”

Naye mchambuzi wa ligi hiyo, Kevin O’Conner, alichapisha kwenye mtandao wa X: “Nimekuwa nikisema hili kwa muda mrefu. Wemby yuko karibu kabisa na futi 7 na inchi 7. Nimewahi kuwa karibu na Boban, Tacko Fall hawa watu ni wakubwa kabisa, lakini Wemby ni mrefu kuliko wote.”

“Kwa hili hongera kwa Spurs wanaelekea kukubali kwamba ana futi zaidi ya 7 na inchi 6, ambacho ndicho kimo chake halisi. Lakini angalau sasa tuko kwenye 7’5”. Kareem (Abdul-Jabbar) aliwahi kusema uongo, Bill Walton aliwahi kusema uongo, (Kevin) Durant naye ni mwongo wa kimo,” alisema mchambuzi wa NBA, Bill Simmons kwenye podikasti yake.

Sio jambo geni kwa wachezaji vijana kuongeza kimo miaka ya awali ya maisha yao katika ligi hiyo kwani nyota wa Milwaukee Bucks, Giannis Antetokounmpo aliwahi kuongezeka.

Akiwa tayari na upana wa mikono wa futi nane, nyota huyo wa Spurs ameongoza NBA kwa “blocks” kwa misimu miwili iliyopita.