Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wembanyama aipeleka Spurs fainali za NBA

WAMBINYANA Pict

Muktasari:

  • Mfululizo wa fainali za NBA utaanza tarehe 3 Juni, huku mchezo wa saba wa uamuzi ukitarajiwa kuchezwa tarehe 19 Juni iwapo timu hizo zitafungana katika michezo sita ya kwanza.

OKLAHAMA, MAREKANI: Nyota Victor Wembanyama alifunga pointi 22 huku San Antonio Spurs ikiibuka na ushindi wa 111-103 dhidi ya mabingwa watetezi Oklahoma City Thunder na kufuzu kwa fainali za NBA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014.

Spurs sasa itakutana na New York Knicks katika mfululizo wa fainali za NBA.

Kabla ya mchezo huo wa uamuzi, kocha wa Spurs, Mitch Johnson alikuwa amemtaka Wembanyama kufunga zaidi ya pointi 20 baada ya kiwango kisichoridhisha alichoonyesha katika mchezo wa tano wa mfululizo huo.

Nyota huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 alikuwa tayari ameonyesha uwezo wake mkubwa katika mchezo wa sita alipofunga pointi 28 na kusaidia Spurs kusawazisha mfululizo huo wa michezo saba kwa matokeo ya 3-3, hivyo kuendelea kuishi kwa ndoto yake ya kutwaa ubingwa wa NBA.

WEMBA 01

Baada ya kufuzu kwa fainali kwa mara ya kwanza katika maisha yake, Wembanyama amesema:“Kushinda Kombe la Larry O'Brien (kombe la ubingwa wa NBA) ni ndoto yangu tangu utotoni. Na sasa kuwa na nafasi halisi ya kulishinda ni fursa ya kipekee  maishani.

“Huwezi kujua nafasi kama hii itakuja tena lini. Lakini siku nitakapolishinda, kwangu binafsi itakuwa siku ya ajabu ya kutimia kwa ndoto yangu.

“Ni vigumu kuelezea kwa maneno. Karibu ni kama maana ya maisha yangu.”

Spurs ilitwaa ubingwa wake wa mwisho wa NBA mwaka 2014, huku Knicks ikirejea kwenye fainali kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27.

Fainali hizi zitakuwa marudio ya zile za mwaka 1999 ambapo San Antonio Spurs iliifunga New York Knicks katika michezo mitano na kutwaa ubingwa wake wa kwanza kati ya mataji matano ya NBA.

Baada ya kufunga pointi 41 katika mchezo wa kwanza na pointi 33 katika mchezo wa nne, Wembanyama ameonyesha katika michezo miwili ya mwisho kwa nini alikuwa mmoja wa vipaji vilivyotafutwa zaidi katika Draft ya NBA ya mwaka 2023, kiwango ambacho wengi walikilinganisha na kile cha LeBron James mwaka 2003.

WEMBA 02

“Nimejifunza ninaweza kuvuka vikwazo vikubwa kuliko nilivyowahi kufikiria,” amesema Wembanyama.

“Nimegundua nguvu ndani yangu, kutokukata tamaa. Nilikuwa najua hilo tayari, lakini kufanya hivyo katika kiwango hiki ni jambo tofauti kabisa.

“Huu ndiyo mpira wa kikapu bora zaidi duniani kwa sasa. Na jambo la kushangaza ni kwamba nataka kufanya hivi mara nyingine 15 au 20 zaidi.”

Mfululizo wa fainali za NBA utaanza tarehe 3 Juni, huku mchezo wa saba wa uamuzi ukitarajiwa kuchezwa tarehe 19 Juni iwapo timu hizo zitafungana katika michezo sita ya kwanza.