Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasaudia ni kufa au kupona kupata saini ya Mohamed Salah

Muktasari:

  • Staa huyu anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi kutokana na kile kinachoendelea kati yake na kocha Arne Slot ambaye hawapo katika uhusiano mzuri kwa sasa.

TIMU za Saudi Arabia zinajipanga kufanya kila linalowezekana kuhakikisha mojawapo inamsajili mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah.

Staa huyu anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi kutokana na kile kinachoendelea kati yake na kocha Arne Slot ambaye hawapo katika uhusiano mzuri kwa sasa.

Salah mwenye umri wa miaka 33, amekuwa katika wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu huu, hali iliyosababishwa awekwe benchini katika mechi kadhaa zilizopita.

Siku kadhaa zilizopita alifunguka kwamba hapendezwi na hali ya kuwekwa benchini na akaweka wazi kwamba haoni kama ataendelea kuwepo Liverpool baada ya dirisha la Januari.

Salah mwenye umri wa miaka 33, amekuwa akiwindwa na timu za Saudia tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini aligoma kuondoka na akaamua kusaini mkataba wa kuendelea kusalia katika kikosi cha majogoo.

Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Antoine Semenyo

LIVERPOOL inatajwa kuwa ndio timu iliyochaguliwa na mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25, licha ya timu nyingine za England, Tottenham, Arsenal na Manchester City kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Semenyo amekuwa akiwindwa na vigogo wengi barani Ulaya tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi. Mkataba wa sasa wa Semenyo unatarajiwa kumalika mwaka 2030. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 15 na kufunga mabao matano.


Marc Guehi

BEKI wa Crystal Palace, Marc Guehi mwenye umri wa miaka 25, ameendelea kuwa katika rada za Liverpool kuelekea dirisha lijalo la majira ya baridi, lakini Barcelona bado imeendelea kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Guehi ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na timu nyingi barani Ulaya ambazo zimevutiwa sana na kiwango chake, pamoja na hali yake ya mkataba ambao unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.


Joshua Zirkzee

ROMA imeanza mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo, Joshua Zirkzee, 24, ili kumsajili katika dirisha la usajili la Januari. Ili kumsaini Roma imepanga kwanza kuachana na straika wa Brighton na timu ya taifa ya Ireland. Zirkzee anahusishwa kuondoka Man United kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha mashetani wekundu hao.


Jack Grealish

KIUNGO wa Manchester City anayecheza kwa mkopo wa msimu mmoja Everton, Jack Grealish, 30, anakusikia furaha katika kikosi cha wakongwe hao wa Jiji la Liverpool na anataka kuendelea kusalia kwa kusaini mkataba wa moja kwa moja mwisho wa msimu. Inaelezwa Grealish anaamini ataendelea kupata nafasi ya kutosha na kuonyesha kiwango bora katika kikosi cha kwanza cha Everton.


Yan Diomande

LIVERPOOL na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kumsajili winga wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yan Diomande, 19,  kuelekea dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti zinaeleza mabosi wa Leipzig wapo tayari kumwachia lakini kwa kiasi kisichopungua Pauni 69  milioni. Mkataba wa staa huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2030. Msimu uliopita alicheza mechi 15 za michuano yote na kufunga mabao saba.


Tiago Gabriel

JUVENTUS imefikia hatua nzuri katika  mazungumzo yake na wawakilishi wa beki kisiki wa Lecce na timu ya taifa ya Ureno kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21, Tiago Gabriel, 20. Juventues inataka kumsajili staa huyu katika dirisha lijalo la majira ya baridi lakini inakutana na upinzani mkali kutoka kwa Brentford ambayo pia inahitaji saini yake.


Marc Cucurella

ATLETICO Madrid inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania, Marc Cucurella ambaye inataka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Staa huyu ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza Chelsea mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.