Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakali wa kutupia 4 mechi 1 EPL

Muktasari:

  • Kwenye matukio adimu, kuna wachezaji hao kufunga bao moja kwenye mechi halikuwa jambo linalowatosha na hivyo kufunga mara nyingi, wengine wakitikisa nyavu mara nne au tano kwenye mechi moja na hivyo kuweka rekodi za kibabe kabisa.

LONDON, ENGLAND: KUFUNGA mabao ni moja ya kazi ngumu sana kwenye soka. Inaweza kushusha morali ya mshambuliaji hasa anapokuwa kwenye kipindi cha kuandamwa na ukame wa kushindwa kufunga mabao. Lakini, kuna baadhi ya washambuliaji, wao kufunga halijawahi kuwa jambo gumu kwao.

Kwenye matukio adimu, kuna wachezaji hao kufunga bao moja kwenye mechi halikuwa jambo linalowatosha na hivyo kufunga mara nyingi, wengine wakitikisa nyavu mara nne au tano kwenye mechi moja na hivyo kuweka rekodi za kibabe kabisa.

Staa wa Chelsea, Cole Palmer amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye historia ya Ligi Kuu England kufunga mabao manne kwenye kipindi cha kwanza cha mechi moja, alipofanya hivyo dhidi ya Brighton, Septemba 28, 2024. Hiyo ilikuwa ni mara ya 32 kwa mchezaji kufunga mabao manne au zaidi kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England tangu ilipoanza kutumia mfumo wa sasa mwaka 1992. Andy Cole alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matano kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England wakati alipoiongoza Manchester United kuichapa Ipswich Town 9-0 mwaka 1995. Cole alifunga mabao 21 kwenye ligi msimu huo, akiachwa nyuma kwa mabao mengi na staa aliyeshinda Kiatu cha Dhahabu, Alan Shearer, aliyetupia nyavuni mara 34 msimu huo.

Shearer alifunga mabao matano dhidi ya Sheffield Wednesday mwaka 1999, na ilipita miaka 10 kabla ya mchezaji mwingine kufanya hivyo. Hakuna timu iliyofunga mabao 10 kwenye Ligi Kuu England, lakini Tottenham Hotspur ilifunga tisa dhidi ya Wigan ya Roberto Martinez mwaka 2009, ambapo kwenye kikosi hicho cha Spurs kulikuwa na staa Jermain Defoe, aliyefunga mabao matano peke yake.

Dimitar Berbatov, mchezaji aliyekuwa bora kabisa kwenye kontroo ya mpira, alikuwa moto msimu wa 2010/11, ambapo alipiga kuanzia tatu kwenda juu dhidi ya Liverpool, Blackburn na Birmingham. Kwenye mechi ya Blackburn hakuishia kwenye kufunga mabao matatu, alifunga matano kwenye ushindi wa 7-1.

Berbatov alifunga kwenye mechi 11 tu kati ya mechi 38 za Man United kwenye ligi, lakini alikwenda kugawana tuzo ya Kiatu cha Dhahabu na Carlos Tevez kwa kufunga mabao 20. Kwa wachezaji watano waliofunga mabao matano kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England ni Berbatov pekee aliyeshinda ubingwa wa ligi hiyo. Gwiji wa Manchester City, Aguero ni mchezaji wa mwisho kufunga mabao matano kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England na hiyo imetokea karibu muongo mmoja uliopita. Aguero alifunga mabao hayo matano ndani ya dakika 20, alipofunga kati ya dakika 42 na 62 kwenye ushindi wa 6-1 ilioupata miamba hiyo ya Etihad dhidi ya Newcastle United.

Hiyo ina maana kuna wachezaji tano tu waliofunga mabao matano kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England. Lakini, kuna kundi la wachezaji wengi sana waliofunga mara nne kwenye mechi moja ya Ligi Kuu England na humo ndani yake kuna mastaa kama Palmer, Aguero, Yakubu, Frank Lampard, Michael Owen, Ole Gunnar Solskjaer na Robbie Fowler, huku wengine wakifanya hivyo kwenye awamu mbili tofauti.

Fowler alikuwa moto mwanzoni mwa maisha yake huko Liverpool, alifunga mabao 30+ kwa misimu mitatu mfululizo kati ya 1994 na 1997, na kilikuwa kipindi hicho ambacho alifunga mabao manne kwenye mechi moja kwa awamu mbili tofauti. Ya kwanza ilikuwa kwenye ushindi wa 5-2 dhidi ya Bolton uwanjani Anfield mwaka 1995, kabla ya kufanya hivyo tena kwenye ushindi wa 5-1 dhidi ya Middlesbrough, pia uwanjani Anfield, mwaka uliofuatia.

Solskjaer alikuwa mchezaji mwingine aliyefunga mara nne kwenye mechi moja, mara mbili tofauti, nne za kwanza ilikuwa dhidi ya Nottingham Forest, Man United iliponyakua mataji matatu makubwa kwa msimu mmoja, 1999. Nyingine ni ile ambayo Solskjaer alitokea benchini katika dakika 72 na kufunga mara nne kuanzia dakika ya 80. Owen alifunga nne kwenye ushindi wa 5-1 dhidi ya Nottingham Forest mwaka mmoja kabla, wakati mabao yake mengine manne akifunga kwenye ushindi wa 6-0 dhidi ya West Brom mwaka 2003. Lampard alifunga nne kwenye ushindi wa 6-1 dhidi ya Derby msimu wa 2007/08 na alirudia kufanya hivyo kwenye ushindi wa 7-1 dhidi ya Aston Villa, ambapo Chelsea ilinyakua ubingwa kwenye msimu wa 2009-10.

Yakubu aliyewahi kuzichezea Portsmouth, Middlesbrough, Everton na Blackburn, alifunga mabao manne kwenye mechi moja akiwa na Portsmouth dhidi ya Middlesbrough mwaka 2004 na ilichukua miaka saba kufanya hivyo tena, alipofunga mara nne akiwa na Blackburn kwenye ushindi wa 4-2 dhidi ya Swansea City mwaka 2011. Aguero anafunga ukurasa kwa wachezaji waliofunga mabao manne au zaidi kwenye mechi moja akifanya hivyo mara tatu tofauti, alipozichapa Tottenham na Leicester mwaka 2015 na 2016 mtawalia. Staa mwingine aliyekuwa moyo ni staa wa Liverpool, Luis Suarez aliyefunga nne dhidi ya Norwich City mwaka 2013.