Wachezaji Nigeria wachelewa kambini, mazoezi yaahirishwa
Muktasari:
- Kwa mujibu wa gazeti le DAILY POST la Nigeria, mazoezi ya kwanza ya Super Eagles leo usiku yameahirishwa, kutokana na idadi kubwa ya wachezaji walioitwa kikosini kuchelewa kufika kambini, huku wachezaji 10 pekee, wakiripoti hadi sasa.
Kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Super Eagles, huenda kikaanza mazoezi ya kwanza leo usiku Novemba 10, 2025, kuelekea mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Gabon itakayochezwa Novemba 13, 2025 saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika mashariki, katika uwanja wa Hide Moulay Hassan nchini Morocco.
Kwa mujibu wa gazeti le DAILY POST la Nigeria, mazoezi ya kwanza ya Super Eagles leo usiku yameahirishwa, kutokana na idadi kubwa ya wachezaji walioitwa kikosini kuchelewa kufika kambini, huku wachezaji 10 pekee, wakiripoti hadi sasa.
Miongoni mwa wachezaji walioripoti kambini ni nahodha William Troost-Ekong, Calvin Bassey, Alex Iwobi, Samuel Chukwueze, na Tolu Arokodare.
Wengine ni Olakunle Olusegun, Wilfred Ndidi, Moses Simon, Benjamin Fredrick, na Chidozie Awaziem.
Hata hivyo wachezaji 14 waliobaki wanatarajiwa kufika kambini baadaye leo Jumatatu, Novemba 10, 2025, hatua ambayo itampa nafasi kocha Eric Chelle, kuanza kusuka mipango yake ya ushindi dhidi ya Gabon.
Kikosi cha Nigeria kilichoitwa kwa ajili ya mechi hiyo kina wachezaji 24 ambao ni:
Makipa: Stanley Nwabali (Chippa United, Afrika Kusini), Amas Obasogie (Singida Black Stars, Tanzania), Maduka Okoye (Udinese, Italia).
Mabeki: William Troost‑Ekong (Al‑Kholood, Saudi Arabia), Calvin Bassey (Fulham FC, England), Oluwasemilogo Ajayi (Hull City, England), Bright Osayi‑Samuel (Birmingham City, England), Bruno Onyemaechi (Olympiakos, Ugiriki), Chidozie Awaziem (Nantes FC, Ufaransa), Zaidu Sanusi (FC Porto, Ureno), Benjamin Fredericks (Dender FC, Ubelgiji), Semi Ajayi (Hull City, England).
Viungo: Alex Iwobi (Fulham FC, England), Wilfred Ndidi (Besiktas FC, Uturuki), Raphael Onyedika (Club Brugge, Ubelgiji), Frank Onyeka (Brentford FC, England), Alhassan Yusuf Abdullahi (New England Revolution, Marekani).
Washambuliaji: Victor Osimhen (Galatasaray FC, Uturuki), Ademola Lookman (Atalanta BC, Italia), Samuel Chukwueze (Fulham FC, England), Moses Simon (Paris FC, Ufaransa), Chidera Ejuke (Sevilla FC, Hispania), Tolu Arokodare (Wolverhampton Wanderers, England), Akor Adams (Sevilla FC, Hispania) na Olakunle Olusegun (Pari Nizhny Novgorod, Urusi).