Vita ya ubingwa EPL bado mbichi
Muktasari:
- Arsenal iliyokuwa uwanjani usiku wa jana ugenini dhidi a Brentford, imejikuta ikisaliwa na pointi tatu tofauti na ilizonazo Man City iliyoshinda jana usiku kwa mabao 3-0 nyumbani mbele ya Fulham na kuzidi kuibana Gunners ambayo usiku wa kuamkia leo ilikuwa uwanjani dhidi ya Brentford
LONDON, ENGLAND: VITA ni kali England. Ndio, Arsenal na Manchester City zipo ktika vita kali ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) zina uwezekano wa kukutana mara tano kuanzia mwezi ujao hadi mwisho wa msimu katika michuano mbalimbali.
Arsenal iliyokuwa uwanjani usiku wa jana ugenini dhidi a Brentford, imejikuta ikisaliwa na pointi tatu tofauti na ilizonazo Man City iliyoshinda jana usiku kwa mabao 3-0 nyumbani mbele ya Fulham na kuzidi kuibana Gunners ambayo usiku wa kuamkia leo ilikuwa uwanjani dhidi ya Brentford
Gunners imeanza kuingiwa ubaridi wa kubeba taji la kwanza la EPL baada ya muda mrefu kupita, kwani ushindi wa juzi umeifanya City ifikishe pointi 53 kupitia mechi 26, huku yenyewe kabla ya mechi ya jana ilikuwa na 56 kupitia mechi 25.
Lakini sasa inaonekana wazi kuna uwezekano wa timu hizo kufanyiziana zaidi msimu kwani ratiba inaonyesha zinaweza kukutana mara tano kuanzia Machi. Kwanza kabisa Mikel Arteta na Pep Guardiola watakutana kwenye fainali ya Kombe la Carabao mwezi ujao na baada ya hapo zinaweza kukutana katika Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mechi hiyo ya Carabao itapigwa Machi, 22, katika dimba la Wembley na baada ya hapo kutakuwa na mechi nyingine kati yao kwenye Ligi Kuu Aprili, 18, inayotarajiwa kuwa na athari kubwa kwenye hatima ya ubingwa.
Hatua ya mzunguko wa tano wa Kombe la FA inatarajiwa kuchezwa kati ya Machi 7 hadi nane, na kuna uwezekano Arsenal na Man City zikapangwa kucheza dhidi ya kila mmoja ama zikakutana katika hatua inayofuata. Pia kuna uwezekano mkubwa timu hizo zikakutana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya zote kufuzu moja kwa moja kwenda hatua ya 16 bora. Kwa mujibu wa kanuni za upangaji wa droo, Arsenal na City haziwezi kukutana katika hatua hiyo, lakini zinaweza kupangwa kuc heza dhidi ya kila mmoja kwenye robo fainali, zitakazochezwa kwa mechi mbili (nyumbani na ugenini) Aprili 7 na 8, huku mechi ya marudiano ikichezwa wiki moja baadaye.
Arsenal mara ya mwisho kutwaa ubingwa wa EPL ilikuwa msimu wa 2003-04, jambo linalowavuruga.
Man City iliendelea kuisogelea Arsenal kileleni baada ya kupata ushindi katika dakika za mwisho dhidi ya Liverpool Jumapili, ambapo ingepoteza ingejikutana imeachwa kwa tofauti ya alama tisa. Guardiola tayari amegusia uwezekano wa Arsenal na Man City kukutana mara nyingi zaidi kabla ya msimu huu kumalizika, akisema:“Inaweza ikatokea. Sijui nini kitatokea kwenye Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu, lakini ratiba ipo. Nitapenda pia hilo ikiwa itatokea, tena nahitaji sana tukutane fainali.”