Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Imefichuka! Arsenal ni wazee kuliko Man United

ARSENAL Pict
ARSENAL Pict

Muktasari:

  • Usibishe. Mtandao wa Transfermarkt unaweka bayana wastani wa umri wa kila kikosi kwenye Ligi Kuu England msimu huu wa 2025/26.

LONDON, ENGLAND: HIVI unajua kuwa Arsenal ni wazee kuliko Manchester United?

Usibishe. Mtandao wa Transfermarkt unaweka bayana wastani wa umri wa kila kikosi kwenye Ligi Kuu England msimu huu wa 2025/26.


Fulham – 27.7

Kikosi cha Fulham kina wachezaji saba tu wenye umri unaozidi miaka 30, wakiwamo Tom Cairney, Bernd Leno na Raul Jimenez. Kuna kundi jingine la wachezaji saba wenye umri wa miaka 25. Fulham haina wachezaji wengi chini ya miaka 20, ni wawili tu Josh King na Jonah Kusi-Asare. Kwa wastani wa umri, kikosi hicho cha kocha Marco Silva kina umri wa miaka 27.7 kwa mujibu wa Transfermarkt.


Aston Villa – 27.3

Kocha Unai Emery amekuwa na mafanikio makubwa Aston Villa tangu alipotua Villa Park. Kwenye Ligi Kuu England, Aston Villa ni moja ya timu yenye kikosi chenye wastani mkubwa wa umri. Kikosi hicho kina wachezaji wanane wenye umri chini ya miaka 25, akiwamo Harvey Elliott, lakini kipa Emiliano Martinez ana miaka 33 akiongoza kundi la wachezaji wenye uzoefu mkubwa, akiwamo Marco Bizot, 34.


Everton – 26.6

Kwa nadharia, kikosi cha David Moyes cha Everton kinapaswa kuwa kilele cha uwezo wao. Wapo wachache wakongwe kwenye kikosi, wakiwamo Idrissa Gueye (36) na Seamus Coleman (37), huku Michael Keane na James Tarkowski wakiwa na miaka 33. Ina vijana pia kama Jarrad Branthwaite (23), Tyler Dibling, Tyrique George na Adam Aznou, ambao bado hawajafikisha miaka 20.


Burnley – 26.5

Burnley, waliopanda tena Ligi Kuu baada ya msimu mmoja tu katika Championship, bado hawajafanikiwa kupata mlolongo wa matokeo mazuri ili kujikwamua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja. Kikosi chao kina Bashir Humphreys (22) na Lesley Ugochukwu (21) huku wazoefu ni Kyle Walker na Martin Dubravka na kufanya kikosi hicho kuwa na wastani wa umri wa miaka 26.5.


Newcastle United – 26.4

Kikosi cha Eddie Howe cha Newcastle United kimejaa uzoefu unaohitajika, wakiwamo wachezaji wanane wenye umri wa 30 au zaidi. Fabian Schar na Kieran Trippier ni mfano halisi. Hata hivyo, wachezaji kama Lewis Miley na Lewis Hall wapo kuhakikisha wastani wa umri uko chini kidogo, sambamba na Tino Livramento (23) na William Osula (22), ambao wanafanya kikosi kuwa na wastani wa umri wa miaka 26.4.


Leeds United – 26.3

Mei 2026, mwisho wa msimu je, Daniel Farke atacheka ama atalia? Wakati utaamua, kama Leeds United, ambayo ina wachezaji 26 kikosini wataweza kuishinda hatari ya kushuka daraja. Kikosi kina wachezaji kama Dominic Calvert-Lewin (28), Noah Okafor (25) na Lukas Nmecha (26), ambao wanaipa timu nafasi bora ya kuendelea kubaki kwenye EPL. Karl Darlow, Alex Cairns na Sam Byram – wote wakiwa juu ya miaka 30 wana uzoefu, huku mdogo ni Facundo Buonanotte, 21.


West Ham United – 26.2

Zamani West Ham United ilihesabiwa kama timu yenye wachezaji wakongwe zaidi Ligi Kuu. Wachezaji kama Lukas Fabianski (40) na Callum Wilson (33). Adama Traore, Tomas Soucek na Alphonse Areola pia wote wapo juu ya miaka 30. Vijana wao ni Mateus Fernandes na El Hadji Malick Diouf, wote wakiwa na miaka 21 tu. Ni mchanganyiko wa uzoefu na njaa ya ujana kikosi kikiwa na wastani wa umri wa miaka 26.2.


Liverpool – 26.1

Arne Slot aliporithi kikosi cha Jurgen Klopp, ilikuwa ni mechi kamili. Kikosi kina mastaa kama Dominik Szoboszlai na Alexis Mac Allister, ambao wapo juu ya miaka 26. Lakini, kuna wakongwe kama Alisson (33), Virgil van Dijk (34) na Mohamed Salah (33), ambao wanafanya miamba hiyo ya Anfield kuwa na kikosi chenye wastani wa umri wa miaka 26.1. Liverpool bado ina timu ya kupambana.


Crystal Palace – 25.9

Selhurst Park ilishuhudia mabadiliko ya kikosi msimu wa joto, huku Crystal Palace ikiagana na Eberechi Eze na kumpokea winga mchanga na mwenye motisha, Yeremy Pino. Ameingizwa kwenye kikosi chenye mvuto, pamoja na kiungo wa England, Adam Wharton, ambaye bado ana miaka 21 tu. Palace ina wachezaji kama Brennan Johnson, Evann Guessand na Jorgen Strand Larsen, vijana wenye njaa ya mafanikio.


Arsenal – 25.6

Mikel Arteta anapaswa kushukuru uti wa mgongo wa kikosi chake kuwa na vijana kwa nafasi ilipo Arsenal katika orodha hii ya wastani wa umri. Wangeweza kuwa chini zaidi, kama hapakuwa na wachezaji wa akademi. Kikosi kimechanganyika wenye umri mkubwa kama Christian Nørgaard (31), Leandro Trossard na Kepa Arrizabalaga pamoja na vijana kama Myles Lewis-Skelly na Max Dowman.


Wolves – 25.6

Kikosi cha Rob Edwards kina mchanganyiko mzuri wa uzoefu na ujana kote uwanjani. Matt Doherty, ambaye kwa miaka mingi amekuwa akionekana na mashabiki wengi kama mchezaji mkongwe wa zaidi ya miaka 30, ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kikosini akiwa na miaka 34 pekee. Timu hiyo inayopambana na hali yake isishuke daraja ina kikosi chenye wastani wa umri wa miaka 25.6.


Nottingham Forest – 25.5

Iwe ni kubadilisha makocha au misukosuko ya mara kwa mara ndani ya kikosi, Nottingham Forest haikosi mabadiliko. Wachezaji kadhaa walisajiliwa ili kuimarisha nafasi yao miongoni mwa timu zinazowania soka la Ulaya, wakiwamo Omari Hutchinson (22), James McAtee (23) na Igor Jesus (24). Forest sasa inajivunia kuwa na kikosi kikubwa zaidi katika ligi baada ya dirisha la usajili la Januari kufungwa.


Brentford – 25.3

Chini ya Thomas Frank, Brentford ilikuwa kati ya timu zilizovutia zaidi kutazamwa, na hilo limeendelea msimu wa 2025/26 chini ya Keith Andrews. Kwa kuvutia sana, wamefanikiwa kudumisha hadhi yao ya Ligi Kuu kwa miaka kadhaa wakiwa na kikosi chenye umri mdogo, hali ambayo imeendelea kuwa sehemu ya utambulisho wao. Jordan Henderson na Ethan Pinnock ni wachezaji wakongwe kikosini.


Brighton – 25.3

Brighton kwa kawaida hutazamwa kama timu changa yenye vipaji vingi, kutokana na sera yake bora ya usajili ambayo imeiwezesha kuleta vipaji vingi vya kipekee katika Uwanja wa AMEX. James Milner, 40, ndiye mkongwe wa kikosi, sambamba na Jason Steele na Danny Welbeck, wote wakiwa na umri wa miaka 35. Lakini, timu ina vijana kama Carlos Baleba, Yankuba Minteh na Jack Hinshelwood.


Man United – 25.2

Ni kweli kwamba kuna baadhi ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika kikosi cha Manchester United kwa sasa. Kipa wa chaguo la tatu Tom Heaton, kiungo Casemiro, na nahodha wa zamani Harry Maguire ni miongoni mwa wachezaji wakongwe zaidi katika kikosi cha Michael Carrick. Hata hivyo, Man United ina wachezaji 12 wenye umri wa miaka 25 au chini, akiwamo Kobbie Mainoo (20) na Amad (23).


Bournemouth – 25.1

Bournemouth, ikiongozwa na kocha anayeheshimika Andoni Iraola, ilikuwa kati ya timu zilizoshangaza wengi katika Ligi Kuu England msimu wa 2024/25, licha ya baadhi ya watu kubashiri klabu hiyo kushuka daraja kabla hata ya msimu kuanza. Mchanganyiko mzuri wa wachezaji uliwasaidia sana, wachache tu walio kwenye miaka ya 30; Fraser Forster (37), Adam Smith (34) na Ryan Christie (30).


Man City – 25.0

Manchester City chini ya Pep Guardiola imeunda kikosi chenye nguvu kubwa, chenye mchanganyiko wa wakongwe na vijana. Wachezaji kama Joško Gvardiol, Phil Foden, na Erling Haaland ni miongoni mwa wanaovutia zaidi, wote wakiwa na umri wa miaka 25 au chini. Kikosi kimeongeza vijana wengine kama Rayan Cherki, Marc Guehi na Antoine Semenyo, wakiwa na umri wa miaka 26 au chini.


Sunderland – 24.8

Ili kuongeza nafasi yao za kubaki kwenye Ligi Kuu, Sunderland, ikiongozwa na Regis Le Bris, ilifanya matumizi makubwa ya fedha wakati wa dirisha la usajili wa majira ya joto, lakini walifanya hivyo kwa busara kwa kuwekeza zaidi kwa wachezaji vijana walioweza kukaa klabuni kwa muda mrefu. Kikosi kina wakongwe kama Reinildo (32) na Granit Xhaka (33) na Nordi Mukiele na Omar Alderete wakikaria 30.


Tottenham – 24.8

Tottenham Hotspur ina wastani wa umri wa 24.8, chini ya uongozi wa Thomas Frank. Baada ya nahodha wa zamani Son Heung-min kuondoka kwenda Los Angeles FC, wastani wa umri wa kikosi ulipungua kwa kiasi kikubwa. Sasa ni wachezaji wawili tu katika kikosi cha wachezaji 28 walio na umri wa miaka 30 au zaidi: Ben Davies na Joao Palhinha. Idadi kubwa ya wachezaji wana umri wa miaka 25 au chini.


Chelsea – 23.4

Kwa kuzingatia idadi kubwa ya wachezaji vijana waliowasajili katika madirisha mawili ya usajili yaliyopita, haishangazi kuona Chelsea ikiwa na kikosi kichanga zaidi katika Ligi Kuu England. Chelsea ndiyo timu yenye wastani wa umri mdogo zaidi kwenye Ligi Kuu England, miaka 23.4.

Idadi kubwa ya wachezaji wakongwe wameondoka, akiwamo Raheem Sterling.