Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vita ya miaka 20 kurejea nusu fainali Kombe la Dunia 2026

WABABE Pict

Muktasari:

  • Kocha Thomas Tuchel ameiongoza England kufikia hatua hii baada ya miaka mingi ya kusaka mafanikio makubwa duniani. Ameunda kikosi chenye nidhamu, uimara wa kiakili na uwezo wa kupambana hadi dakika za mwisho.

ATLANTA, MAREKANI: BAADA ya kusubiri kwa miaka 20, moja ya ushindani mkubwa na wenye historia ndefu katika soka la kimataifa unarejea tena huku England ikipambana na Argentina katika Uwanja wa Atlanta kuwania tiketi ya kufuzu fainali ya Kombe la Dunia 2026.

Kocha Thomas Tuchel ameiongoza England kufikia hatua hii baada ya miaka mingi ya kusaka mafanikio makubwa duniani. Ameunda kikosi chenye nidhamu, uimara wa kiakili na uwezo wa kupambana hadi dakika za mwisho.

Kwa upande mwingine, Argentina, mabingwa watetezi wa dunia chini ya Lionel Scaloni, wanaingia katika mchezo huu wakiwa na rekodi ya asilimia 100 ya ushindi kila walipofika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia. Timu itakayoshinda itakutana na mshindi kati ya Ufaransa na Hispania katika fainali itakayopigwa East Rutherford.

JAMBO Pict

Safari zao

England imeonyesha moyo wa kipekee katika hatua za mtoano. Baada ya kumaliza kileleni mwa Kundi L na kuiondoa DR Congo, iliwashangaza wenyeji wenza Mexico kwa ushindi wa mabao 3-2 katika hatua ya 16 bora kwenye Uwanja wa Azteca.

Katika robo fainali dhidi ya Norway huko Miami, England ilijikuta nyuma lakini Jude Bellingham aliibuka shujaa kwa kufunga mabao mawili katika muda wa nyongeza na kuipa timu ushindi wa 3-2. Ushindi huo uliifanya England kufunga angalau mabao mawili katika mechi nne mfululizo.

Argentina nayo imepitia safari yenye changamoto nyingi. Baada ya kutawala kundi lake, ilifanya moja ya marejeo makubwa kwa kuifunga Misri mabao 3-2 kabla ya kupata upinzani mkali kutoka Uswisi katika robo fainali.

Baada ya sare ya dakika 120, Julián Álvarez aliifungia Argentina bao la ushindi katika muda wa nyongeza na kuwapa ushindi wa 3-1 dhidi ya Uswisi waliokuwa wamebaki na wachezaji 10. Matokeo hayo yaliifanya Argentina kufikisha mechi 12 mfululizo bila kupoteza katika Kombe la Dunia tangu mwaka 2022.

KISASI Pict

Matumaini, majonzi

England bado inaendelea kukabiliwa na changamoto upande wa beki wa kulia. Jarell Quansah anatumikia adhabu ya kusimamishwa, huku Reece James akiwa na uwezekano mdogo wa kuanza kutokana na majeraha yake ya mara kwa mara. Hivyo Ezri Konsa au Djed Spence wanaweza kupewa nafasi ya kuanza.

Kwa Argentina, Lionel Scaloni ana kikosi kilicho katika hali nzuri kimwili. Changamoto yake kubwa ni kuchagua kati ya Julián Álvarez na Lautaro Martínez watakaoanza sambamba na nahodha Lionel Messi.

Mchezo huu pia utakuwa muhimu katika mbio za Kiatu cha Dhahabu (Golden Boot). Messi anaongoza kwa mabao manane, huku Harry Kane na Jude Bellingham wakimfuatia kwa mabao sita kila mmoja.

TUCH 03

Vita ya kiufundi

Mapambano ya katikati ya uwanja yanatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kuamua mshindi.

Messi anatarajiwa kushuka katikati kutafuta nafasi, akisaidiwa na Enzo Fernández pamoja na Alexis Mac Allister katika kuanzisha mashambulizi na kutengeneza nafasi dhidi ya safu ya ulinzi ya England.

Kwa upande wa England, Declan Rice na Kobbie Mainoo watakuwa na jukumu la kuzuia upatikanaji wa pasi kuelekea kwa Messi na kuifanya Argentina ishindwe kujenga mashambulizi kwa urahisi.

England pia itategemea uwezo wa Jude Bellingham kuanzisha mashambulizi ya kushtukiza na kumtafutia nafasi Harry Kane ndani ya eneo la hatari.

TUCH 02


Ulinzi Utakaobeba Matokeo

England italazimika kuboresha safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao katika hatua za mtoano. Makosa yoyote dhidi ya safu kali ya ushambuliaji ya Argentina yanaweza kugharimu.

Kwa Argentina, Cristian Romero pamoja na beki mwenzake watakuwa na kazi kubwa ya kumdhibiti Harry Kane na kuhakikisha Jude Bellingham hapati nafasi ya kupenya kutoka safu ya pili.


Takwimu Muhimu Kabla ya Mechi

*Huu utakuwa mchezo wa sita wa England na Argentina kukutana katika historia ya Kombe la Dunia.


*England inaongoza rekodi ya ushindi kwa kushinda mara tatu dhidi ya ushindi mbili wa Argentina.


*Miongoni mwa mechi maarufu kati ya mataifa haya ni robo fainali ya mwaka 1966, mchezo wa "Hand of God" wa Diego Maradona mwaka 1986, pamoja na pambano la hatua ya 16 bora mwaka 1998.


*Argentina imefika nusu fainali ikiwa imeshinda mechi zote za mashindano haya bila kupoteza hata pointi moja.


*Lionel Messi anaongoza mbio za wafungaji kwa mabao nane.


*England chini ya Thomas Tuchel imeonyesha uthabiti mkubwa katika hatua za mtoano, huku Harry Kane na Jude Bellingham wakiwa wamefunga mabao sita kila mmoja.